Ni ukweli usiopingika kuwa dunia imebadilika sana, vijana wa miaka ya 80-90 ni tofauti na wa miaka ya '00-'20, changamoto zimekuwa nyingi, hasa swala la kukutana na "Mr/Miss right". Wengi wanalalamika kuwa maisha ya "ubize", nyumbani-ofisini-nyumbani na weekends ni nyumbani-kanisani-nyumbani yanawafanya wakose mda wa kukutana na watu 'potential'.
Ndio maana kuna haja ya vijana na wale wanaohitaji kutafuta/kukutana na wenza kuwa na options nyingi, options hizi zaweza kuwa matchmaking(rafiki akukutanishe na rafiki yake, mchungaji akukutanishe na mmoja wa washiriki wa kanisa lake, etc), mitandao kama jamii forums, Facebook
na mingine mingi. Kwa wale ndugu zangu wanaoogopa kuwa-approach wanawake, hizi mbinu ni nzuri sana kwao, coz either rafiki ataunganisha, then wewe utamaliza au simu/mitandao mtaongea wee, then siku mkikutana angalau hofu imepungua.
Sasa tuangalie mbinu sahihi za kufanya online dating iwe na manufaa kwako, kupunguza kuumizwa au kufanywa kipoozeo cha ngono na wenzako.
1. Tafuta websites au forums zenye ubora. Kwa hapa kwetu unaweza kutumia jamii forums, facebook, sina uhakika na instagram. Sio kila website inafaa kuanzisha dating, zingine ni kwa ajili ya biashara ya kuuza na kununua.
2. Kwa forum kama hii, huwezi kumfahamu mtu kiurahisi vile tunatumia fake IDs na picha, hivyo kuwa makini sana. Lakini ukianzisha maongezi, usilazimishe na usipende kuongelea ngono wakati wote, in fact ngono isiwe mada kabisa. Utaweza kumsoma mtu kwa kile anachoandika, utafahamu ABC zake. Kumekuwa na tabia ya kutuma picha za utupu, don't do that, mtu anayejielewa hatumi picha zake za utupu hata siku moja.
3. Usiwe muongo, uongo ni tabia mbaya na wengi wakishagundua wewe ni muongo, watakupotezea hapo hapo. Sema ukweli, hata kama unadhani hilo jambo halitamfurahisha mlengwa.(hapa wengi tunafeli)
4. Ukiona kuna chemistry(mnashabihiana), hamieni kwenye whatsapp/sms na hapo unaweza kuomba/kubadilishana picha.
»Endeleeni kuchat na huku ukijitahidi kufahamu aina ya mtu mliyekutana mtandaoni.
»Unaweza kuomba kupiga simu na mkaongea live(kumbuka sauti humtoa nyoka pangoni )
5. Baada ya maongezi(naamini hapa kila baada ya kazi mtaongea, mtajuliana hali asubuhi na mtatakiana usiku mwema), omba mkutane, kubali kukutana kama hisia zako zinakuruhusu(kama unahisi ile chemistry inazidi kukua, kama sivyo mwambie mda bado avute subira kwanza) .
»Usipende kukutana na mtu sehemu iliyojificha, huko ndani ndani wala sehemu iliyo wazi sana.
»Wengine siku ya kwanza wanakutana hotel, wanachukua chumba kabisa, hiyo sio dating hapo mtakuwa mmefanya arrangement ya sex, ile inayofanywa kwenye sites za kuuza na kununua, mkibwagana/ukibwagwa unaanza kulalama.
»Kutaneni mchana au jioni, epukeni kufanya dating ya kwanza usiku. Hii ni faida kwa usalama wako, huwezi kujua unakutana na kiumbe gani, wengine ni serial killers.
»Dating ya kwanza sio mahala pa kula kuku mzima, bia/Heineken kumi, nk. Ni sehemu ya kunywa soft drinks, chai, kahawa na bites. Mkinywa vilevi huenda mambo yakaharibika.
»Kama unahisi hakuna la maana(yule uliyedhani ndiye-siye), usipoteze mda sana, unaweza kuomba excuse baada ya maongezi mafupi, lakini hakikisha you don't turn him/her off
»Kumbuka, huendi kukutana na malaika, usiweke matarajio makubwa kupitiliza, he/she's just a human being, mwenye udhaifu mwingi tu.
6. Naamini baada ya hapo mtakuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kudate au kuacha kudate kulingana na hisia zenu. Binafsi naamini kumwambia mtu ukweli, kama unaona hana sifa ulizohitaji, ni heri kumwambia ukweli ili aanze upya, usimtumie na kumuumiza hisia then umuache.
Muhimu, mkiachana yaishie pale, hakuna haja ya kumtangaza wala kumsema kwa rafiki zako
»Dates zinazofuata mtaamua mkutane wapi na mda gani(bado nasisitiza kukutana sehemu ya wazi na sio usiku, hapo ndio maswala ya ngono hupewa hisia(kuyaongea), mkubaliane kama it's the right time or not, au muangaliane tu hadi ndoa, hilo ni juu yenu.
NB; Wale wanaoona online dating is Upumbavu, Ujinga na Udomo zege, hii thread itakuwa haiwahusu. Wao waendelee kumuomba baba mchungaji awakutanishe na wapendwa wao
Mwisho, Mshirikishe Mungu, omba sana coz hii ni changamoto kubwa kwa wadada na wakaka wa leo.
By Eli79