Sitti alisema wakati Rais Magufuli alivyoagiza wasio na vyeti wachunguzwe, aliamua kurudi chuoni nchini Marekani kwa ajili ya masomo na kupata vyeti kwa ajili ya kumsaidia kuendesha harakati alizokuwa amezianzisha baada ya kupokwa taji la Miss Tanzania kwa madai ya kudanganya umri mwaka 2014.
Sitti, ambaye alifanikiwa kushinda taji hilo kisha ushindi wake kutenguliwa na kupewa aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa, kimya chake cha muda mrefu kitafikia kikomo hivi karibuni, atakapoendeleza harakati zake, ikiwamo uandishi wa kitabu chake cha Chozi la Sitti ni Kampuni yake.
“Kimya changu kwa muda mrefu ni kutokana na kurudi masomoni Marekani kisha kupata vyeti, lakini kwa sasa nimeshamaliza na mambo mbalimbali yataendelea, ikiwamo uzinduzi wa taasisi yangu ya Sitti,” alisema Sitti.
kichwa cha habari na habari ni tofautiiiiii!!!!!!!.Sijui ndo nini?
ReplyDelete