UCHIMBAJI Kokoto Wapigwa Marufuku Kunduchi
0
July 31, 2017
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imependekeza eneo la Kunduchi Machimbo lirasimishwe kuwa eneo la makazi.
Taarifa ambayo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mipangomiji Manispaa ya Kinondoni, Maduhu Ilanga, inasema kwamba eneo hilo lilimilikishwa kwa wachimbaji mbalimbali ambao walimilikishwa kwa kupatiwa leseni za uchimbaji wa kokoto na mawe.
"Eneo hilo lilikuwa na leseni za uchimbaji na leseni zake ziliisha Machi 30, 2010,'' inasema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inasema kwamba Machi, 2006,Serikali iliamua kupiga marufuku shughuli za uchimbaji wa kokoto na mawe katika eneo la machimbo la Kunduchi, uamuzi huu wa Serikali ulifikiwa baada ya kudhihirika kuwa kulikuwa na uchimbaji usiozingatia sheria ukiendelea na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo Barabara Kuu iendayo Bagamoyo.
Tags