UKWELI Mchungu...Bongo Tatizo sio Elimu zetu Tatizo ni sisi Kushindwa Kuwaza nje ya Box

Mpaka sasa nazani hatujaelewa kwa nini Wakina Bil wali Drop Chuo.

Wakina Mark Zuckerberg.

Hawa jamaa na wengine wengi wao tiyari wakiwa vyuoni walisha anza kuwaza nje ya wanavyo fundishwa.

Wenzetu akisha anza kuwaza nje ya anacho fundishwa Haraka haraka husepa ili asipoteze muda yaani Walimu wanafundisha kuelekea Kusini wao wanawaza kuelejea Kaskazini.

KIBONGOBONGO SASA

Sosi tunaamini kwamba ukisomea Udakitari basi piga ua galagaza unapaswa kwenda kuwa Dakitari.

Ukisomea IT basi lazima uwe na laptop yao na ofisi.

Ukisomea Animal sayansi basi unapaswa kuwa kwenye mifugo.

Ukisomea Procurement lazima uwe kwenye Mastoo kama afisa Ugavi.

HATUELEWI HAYA

Dakitari wa Binadamu anaweza maliza na kaanzisha kampuni yake ya Usafiri wa mabasi ila katika usafiri wa mabasi mbele ya safari akaamua kuja kivingine na mabasi ya kubebea wagonjwa pekee yaani mabasi yenye vitanda.
Atatumia sehemu ndogo alio fundishwa hasa kwenye kusafirisha wagonjwa.

Kwamba IT anaweza kuuza karanga lakini kwenye kuuza akaona Adevelop Program au njia ya yeye kuuza karanga kwa utofauti kabisa.

Kwamba Animal Sayansi anaweza baada ya kuhitimu akafungua Microfinance yake ya kutoa mikopo lakini yeye kwa sababu alisomea Nutrion ya Mifugo ili kutatua changamoto za mifugo akawa anatoa mikopo kwa wafugaji wa mifugo pekee ili wanunue vyakula vya mifugo. anafanya hivyo kwa sababu anajua fika mambo ya nutrion na shida wanayo pata Mifugo.

Kwamba Dakitari wa Binadamu baada ya kuhitimu anaweza kwenda kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji na kwenye kilimo akalima mazao pia ya kuweza kuwasaidia wagonjwa na akawa anawauzia sana wagonjwa na kwa sababu ana Idea za nutrition ya binadamu..

Hapo ndo kukariri kunapo chukua nafasi kubwa sana ye Elimu zetu.

KUFIKIRI TOFAUTI NI DHAMBI KUBWA MNO KWA SISI WASOMI

By Chasha Poultry Farm
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad