UKWELI Mchungu...Nani Anaweza Kusimama na Kuyapinga Maneno ya Tundu Lissu yote Aliyoyaongea Kuhusu Serikali


Nani anaweza kusimama na kuyapinga maneno ya Tundu Lissu yote aliyoyaongea kuhusu serikali juzi  ?

Hadi sasa wanaojitahidi kuipinga kauli za Lissu juzi hawajamjibu wala kuonyesha uongo wa kauli zake zaidi wanatoa maneno ya kusutana  , msemaji wa serikali hajamjibu kisomi na   Zitto Kabwe nae amaengukia humo humo kujibu kwa kusuta badala ya hoja.

Lissu ajibiwe kwa hoja siyo vijembe.
By PRODA LTD/JF

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tunachotaka ni majibu tuhuma hizo ni zakweili au laa ?.naona hata bwana mkubwa kapigwa gazi haliongelei hili walete majibu sio ngojera na vitisho.

    ReplyDelete
  2. Unajua watanzania wa sasa ni werevu sana tumeshaelewa na tumejuwa na hatudanganyiki .viva waarma ukweli

    ReplyDelete
  3. Mtoa mada au hoja kwamba nani anaweza kusimama na kupinga maneno ya lisu juu ya serikali? Ina maana wewe unaafiki na kuungana na Lisu kwamba Tanzania inastahiki kutengwa na kukatiwa misaada na jumuia za kimataifa? Ni juzi tu sio mbali tulishuhudia mashirika makubwa yanayojishughulisha na utalii duniani kuitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi bora kabisa barani Africa kwa vivutiyo vya utalii. Wageni wanatupigia debe ili tukubalike duniani la kushangaza wakati baadhi yetu humu ndani tena wanajiita wanauchungu na hii nchi wanahangaika kuzishawishi jumuia za kimataifa tususiwe? Lisu si tu mchochezi bali ana kosa la kuwa ni muhujumu wa uchumi kutokana na kampeni zake za makusudi za kutaka nchi inyimwe misaada ya maendeleo. Vile vile kwa kitendo chake cha kupinga serikali isilishughulikie suala la wizi wa mchanga wa dhahabu. Nchi ipo katika vita vya kiuchumi kitendo cha yeye Lisu kupinga waziwazi mikakati hiyo tayari ameshajiweka katika kundi la maadui. Kuhusu hoja yake yakuwa Magufuli ni mkabila? Mwalimu Nyerere alishasema ukimuona mwanasiasa au chama cha siasa wanatafuta kiki kwa chokochoko za kikabila basi hao ni wakuogopwa kama ukoma. Lets be honest and as clear as clean water. Mtanzania gani mwenye akili timamu asiejua yakuwa Chadema ni Chama kilicho simama katika misingi ya ukabila na ukanda? Watanzania sio kama hawajui na si wapumbavu lakini sio utamaduni wetu kama watanzania kuzungumzia ukabila hazarani ukiachilia mbali masuala ya utani . We ukifuatilia wakati mwengine hata kama kiongozi wa Chadema mfano katika eneo la chato basi kuna uwezekano mkubwa kabisa yakwamba kuwa kiongozi huyo asili yake ni kutoka kaskazini mwa chi yetu na kwanini iwe hivyo? Kama si ukabila kitu gani? Hata watoa hoja na mada na hata maoni mitandaoni wanaoipinga serikali wengi wao hufanya hivyo sio kwa uchungu wa nchi bali husukumwa na hulka za kikanda kupitia vyama wanavyovishabikia kwa maoni yangu ukijungundua kuwa na tabia ya namna hiyo ni bora kubadilika kwani zama hizi za Maghuful utateseka sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Andiko lako halijajibu maswali kutoka kwenye kauli za Lisu.
      1 . Je ni kweli Rais anaongoza nchi kwa misingi ya Kikanda/ Kifamilia / Kikabila ( IGP,AG,Mkuu wa majeshi etc.)
      2. Je nikweli watoto wa dada wamekepewa madaraka makubwa / Nyeti kwa msingi ya upendeleo?
      3. Je ni kweli rais anaingilia uhuru wa mahakama/ Ma jaji?
      4. Je ni kweli Raisi anakandamiza uhuru wa habari kwa kuunga mokono/ kutokemea uvamizi wa kijeshi uliofanywa kweny kituo kimoja cha televiseni? Na badala yake kumpa nishani mvamizi?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad