Ulinzi Aliyoingia nao Wayne Rooney Uwanja wa Taifa leo

Baada ya kikosi cha Everton cha England kuwasili Tanzania asubuhi ya July 12, jioni walifanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kucheza dhidi ya Gor Mahia Alhamisi ya July 13 2017 katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Miongoni mwa mastaa wa Everton waliyowasili katika mazoezi alikuwa ni Morgan Scheiderlin na Wayne Rooney ambaye yeye alionekana kuwekewa ulinzi zaidi wa pekee yake wakati akielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya kuanza mazoezi.

Rooney ambaye katika kikosi cha Everton ndio mchezaji mwenye jina kubwa kuliko wote, aliingia na walinzi watatu wakiwa wanamlinda ili asipate ghasia yoyote, Rooney amejiunga na Everton msimu huu akitokea Man United lakini ni nahodha pia wa timu ya taifa ya England.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad