“Unaweza Kuwadanganya Watu Wachache Muda Wote, Lakini Huwezi Kuwadanganya Watu Wote Muda Wote”
Mh Tundu Lissu aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya uchochezi aliachiwa tarehe 27 Julai 2017 baada ya kupata dhamana. Mh Tundu Lissu alipata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari na alieleza mambo kama manne. Kwa haki hiyo hiyo ya kikatiba anayoidai Mh Tundu Lissu nimeona na mimi ni vyema nitoe maoni nyangu kuhusu aliyoyaeleza au aliyodai.
Kwanza kabisa Mh Lissu amedai kwamba siyo kosa kuikosoa serikali na siyo kosa kueleza uovu wa serikali iliko madarakani na siyo kosa kuikemea serikali iliyopo madarakani. Pia ameeleza kwamba vyama vya upinzani vina haki ya kuwakosoa, kuwasema na kuwakemea watawala kwa sababu ipo sheria ya Vyama vingi inayotoa haki hiyo.
Ni kweli Nchi yetu ilikubali mfumo wa vyama vingi vya siasa na ipo sheria ya Vyama vingi vya siasa inayoeleza pamoja na mambo mengine haki ya kuikosoa serikali na haki ya kufanya mikutano ya siasa na maandamano.
Nimefuatilia kwa muda sasa hotuba za Mh Tundu Lissu bungeni na kwenye mikutano ya hadhara na anapoongea na vyombo vya habari. Mh Tundu Lissu haikosoi serikali bali anatukana au anatumia lugha ya kuudhi kwa viongozi wa nchi au wa vyama vingine. Mh Tundu Lissu anatumia lugha ya jeuri na kutakabari na majivuno anapotoa maoni au ushauri wake.
Lengo la kuruhusu vyama vingi vya siasa ni kupanua wigo wa majadiliano ili kuruhusu maoni au ushauri kutoka kwenye vya siasa vyenye mitazamo tofauti, kwani Papa pamoja na mkulima ni bora kuliko Papa pekee. Kuna sheria ya vyama vingi vya siasa lakini pia ipo sheria ya maadili ya viongozi na pia kama Taifa tuna utamaduni wetu.
Mh Tundu Lissu anataka watanzania waamini kwamba anaonewa kwa sababu yeye anaikosoa serikali na anaeleza uovu wa watawala tu kama sheria ya vyama vya siasa inavyotaka. Mh Lissu anadaganya. Mh Lissu anatumia lugha ya kuudhi na anatukana serikali. Mfano hata Polisi hawaheshimu. Mh Lissu alisema ameambiwa na Lipolisi moja tena likubwa kwamba Lowassa atapelekwa mahakamani. Hiyo ni dharau kwa Polisi. Mh Lissu analidharau Jeshi la Polisi, anamdharau Mh Rais ambaye anaridhaa ya watanzania. Mh Tundu Lissu anasema hatanyamaza kwa sababu nchi inaangamia. Mh Tundu Lissu anataka kuwadanganya watanzania.
Je hatua anazuchukua Mh Rais JPM kupigania rasilimali za nchi ili ziwanufaishe watanzania zinaliangamiza Taifa ?
Je hatua alizochukua Mh Rais JPM dhidi ya mafisadi wa Escrow, mafisadi Bandarini zinaliangamiza Taifa ?
Je Hatua anazochukua Rais dhidi wa wabadhirifu wa mali ya umma na wazembe na wale wanaojinufa kutokana na madaraka waliyonayo zinaliangamiza Taifa ?
Je hatua alizochukua Mh Rais JPM kwenye elimu na hatua za kuhakikisha fedha zinatumika kama ilivyopangwa zinaliangamiza Taifa ?
Je hatua alizochukua Mh Rais JPM kutetea wanyonge na maskini ni uovu ?
Je hasira na ghazabu anazozionyesha Mh Tundu Lissu mpaka amwite Mh Rais ni dikteta uchwara zimesababishwa na kutoandamana tu ?
Mh Tundu Lissu amedai kwamba Mh Rais anawagandamiza watanzania ili aendeshe nchi anavyotaka. Huu ni udanganyifu mwingine. Wakati wa kampeni , CCM na vyama vingine vya siasa vilikuwa vinanadi ilani zake za uchaguzi. Watanzania wengi wakaipenda ilani ya CCM na wakamchagua JPM kuwa Rais. JPM anaongoza serikali inayotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM haendeshi nchi kama anavyotaka.
Mh Tundu Lissu amesema hatanyamaza kwa sababu anapigania haki. Je haki ya kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ?
Lakini pia Mh Lissu atambue yupo Amiri Jeshi Mkuu aliye na dhamana ya kuhakikisha nchi yetu ina amani. Na Amiri Jeshi Mkuu anatambulika na Katiba pia. Hivyo, Vyama vya siasa vitakapotoa taarifa Polisi ya kutaka kufanya mikutano au maandamano. Jeshi la Polisi linaloongozwa na Amiri Jeshi Mkuu ambae ni Rais likiona si vyema mikutano isifanyike au maandamano yasifanyike litatoa taarifa kueleza kuzuia maandamano au mikutano. Maana yake hapa ni kwamba kila mtu anatimiza wajibu wake kikatiba. Anayetaka mikutano na maandamano na anayehakikisha amani ya watanzania. Mazingira ya maelewano yanahitajika na wala siyo ugonvi. Mh Lissu pia anatakiwa aliheshimu Jeshi la Polisi na Amiri Jeshi Mkuu. Huwezi ukamtukana Amiri Jeshi Mkuu halafu unapeleka taarifa kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo huyo uliyemwita Dikteta akuruhusu ufanye shughuli zako na akulinde ili ufanye shughuli zako kwa amani. Papa na mkulima ni bora kuliko Papa pekee. Mh Lissu alitendee haki Jeshi la Polisi pia.
Ningependa watanzania wajiulize Je Mh Lissu anapigania haki ya kutoa maoni na kukemea maovu ndani ya Chadema ? Kwa sababu uovu ni uovu tu. Wengi wanafahamu kuna watu wananyimwa haki ya kukosoa ndani ya Chadema. Mfano, Mh Zitto alipoonekana kutofautiana na uongozi ndani ya Chadema aliitwa msaliti na alikiiona cha mtema kuni. Kafulila pia. Mbona Mh Lissu hajamwita kiongozi yoyote ndani ya Chadema dikteta uchwara ? Mbona Mh Lissu hajapiga kelele juu ya ukabila na kanda ndani ya Chadema ?. Mh Lissu anadai anapigania demokrasia ambayo imeminywa na serikali ya CCM. Iko wapi demokrasia pana ndani ya Chadema wakati uteuzi wa wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki ulidhihirisha pasipo shaka kwamba kulikuwa na udikteta uliopitiliza ? Je Mh Lissu alikemea kuminywa kwa demokrasia wakati wa mchakato ? Je mchakato wa uteuzi wa mgombea urais wa Chadema wa mwaka 2015 ulikuwa wa kidemokrasia ? Gia ilipobadilishwa angani Je Mh Lissu alikemea hilo ? Mh Lissu anadaganya kwamba anapigania haki, siyo kweli Mh Lissu anapigania maslahi yake au kuna watu wanaomtumia.
Wahenga walisema, urais haubadilishi tabia ya mtu bali huidhihirisha. Ni kweli. Mh JPM Rais wa Tanzania amekuwa waziri kwa miaka 20. Watanzania hawakumjua kama ana tabia ambayo kwa sasa inaonekana wazi. Mh JPM amekuwa Rais na sasa ana miaka 2 na tabia yake imeanza kudhihirika. Mh JPM amejulikana si Tanzania pekee bali Afrika Mashariki na Dniani kote. Tabia kuu ya Mh JPM iliyodhihirika wazi ni tabia ya kupenda kutetea watu maskini na kuchukia ufisadi na aina yoyote ya dhuluma. Ni tabia yake ambayo ameiishi na siyo ya kuiga. Miaka 20 iliyopita watanzania hawakuijua tabia hii ya Mh JPM.
Mh Lissu nimemfahamu kuanzia miaka ya 90 akiwa mwanasheria wa LEAT. Wakati huo Mh Lissu hakuwa na lugha hii inayoonekana leo. Lissu alipokuwa Mbunge tabia yake iliaanza kudhhirika. Mtakumbuka hoja zake Mh Lissu kuhusu Muungano. Hivi karibuni Mh Lissu amekuwa Rais wa Shirika la wanasheria Tanzania. Mh Lissu tabia yake kwa sasa iko wazi kwa kila mtanzania. Hamweshimu Rais, Jeshi la Polisi na amesema anakamatwa kwa kuwa ana aklili za kutosha. Anadaganya. Tabia yake iko dhahiri. Mh Lissu ni jeuri na mbishi na anaona yeye tu yuko sahihi na hawezi kunyenyekea. Lakini ni kanuni ya dunia hii kwamba huwezi ukawa kiongozi bila kukubali kuongozwa kwanza. Mh Lissu anawadanganya watanzania kwamba anapigania demokrasia na haki, lakini muda utafika watanzania wengi watatambua kwamba anapigania maslahi yake na kikundi cha watu.
Huwezi ukawadanganya watu wote wakati wote, lakini unaweza kuwadanganya watu watu wote kwa muda
By Fred Mpendazoe
Napingana na uanfishi wako. Uandishi wako pia wakichochezi. Sijakusikia hata siku moja kuandika kutumia lugha hii kwa raisi. Na waandishi kama nyinyi pia ni wapotoshzji. Watu wengi wasomi wasio waoga, wanaozijua sheria hski wanamuunga mkono mbowe. Ccm inajiunga kwa namna nyingine kuposha watu. Kwa mfano leo ngugu ndungai kaungwa mkono na maspika wa sadek, ni baada ya wanasheria wa sadec na wanasheria wa afrika mashariki pia ambao wanazijua sheria kumuunga mkono lissu. Ni kama mchezo wa kipumbavu unachzwa, na wengi wenye akili fupi na wazito kuelewa wanababaiswa. Unamchambua Lisu, na waandishi inabidi muandike facts mnavyozielewa. Ndio huwezi kudanganya wengi au watu wengi.skini hujijui kuandika kwako unawadanganya watu wenye akili zso timamu, wazalendo, wapenda haki. Tumewana pia polisi walivyonyima haki hata mawskili kuzungumza na magazeti. Walivyomzingira bi karume kumnyanyasa kila alikokwenda, unafikiri watanzsnia hawakuliona hili. Unaitetea serikali ukijua wazi lissu anatoa elimu kwa wote mjue haki zenu. Wangapi wsmepotea kwa namna hii, kama mtu anayejua shria na mwanasheria bi Karume anafanyiwa kama alivyofanyiwa sembuse watu wa kawsida si wataswrkwa tu na kuozea huko rumande. Video watu wameziona. Usizungumze uongo kwani watanzania wamejionea wenyewe na inatisha. Wengi hawatasema kitu, bali waacheni wstanzania waamue wenyewe wanayoyaona badsla ya kuwapa maneno ya uongo na uchochezi kupitia uandishi kama huu. Rudi tena shule ujue kuandika vizuri na kutoa habari ilivyo.watanzania wa leo si wsle wa zamani.tunaona.tunasikia. tunatambua.
ReplyDeleteMBONA UNA STORI ZA KIPUMBAPUMBA??
Delete