UVCCM yawajibu CHADEMA kuhusu kauli ya Mzee Mwinyi

Siku chache baada ya Baraza la Wazee wa CHADEMA kutoa tamko kulaumu kauli ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi juu ya maoni yake kuhusu Serikali ya Awamu ya Tano, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wasema Mzee Mwinyi hakukosea.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amesema kauli ya Mzee Mwinyi imetokana na utendaji wa kuvutia na uchapakazi mzuri wa Rais Magufuli na ni maoni yaliyotolewa wazi bila kushurutishwa na mtu bali ni mawazo yake kama Mtanzania.

“Ni ukweli usiofichika kwamba maoni ya Mzee Mwinyi bila shaka yoyote yameenda moja kwa moja kutokana na kuvutiwa na uchapakazi wa Rais Magufuli. Pia maoni hayo hayakuwa ni uwamuzi wala kushurutishwa na mtu bali ni mawazo yake kama Mtanzania na kama Mwananchi mwingine.

“Maoni ya Mzee Mwinyi yalikuwa bayana au unaweza kusema mubashara yanayoweza kumlazimisha kila binadamu mwenye akili timamu hafahamu kwa kila alichotamka katika matamshi yake. Alichokisema ni jambo lenye mantiki baada ya kuaangalia hatma ya Taifa na uzalendo wa Taifa.” – Shaka Hamdu Shaka.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyinyi Vijana jiangalieni sana na msitumike kuligawa Taifa hili kwa kuwaziba watu midomo wanapotoa hoja kuu ambazo ndizo zimetupeleka huko. Na CCM na viongozi wote wahusika wanatokea CCM. Badala ya kuwa zatiti na kusafisha huu uchafu ambao umesababishwa na chama chenu bado mnawakingia kifua wahalifu wakuu waliotusababishia hasara kubwa. Nawashangaeni sana. Na kama mtaendelea kuziba midomo watu wenye nia njema ya kukomesha haya mambo, mkawapaka mafuta matakatifu viongozi wote wakuu waliotusababishia hii mikataba mibaya, basi Tanzania imekufa. CCM haijakiri makosa hata, CCM haizungumzii ni nani mharifu mkuu tuliyempa dhamana ya nchi hii kwa miaka ishirini, na Mnamkumbuka Mwalimu Nyerere kiuongo, ambaye alituambia Watanzania Ybepari ni unyama. Mtazame urefu wa makucha yake na ukali wa meno yake ambao maraisi wetu wameungana na kuwakaribisha mabepari wakuu kutuibia raslimali za mabilioni zikiondolewa kila siku kukicha na viongozi wanaziona leo mnakataa kuwahusisha kwenye migogoro halafu mnamsifia mtu anayejaribu kusafisha na hata Watanzania hatujui ni maneno, ngonjera, au nimbo za lele mama. Toka hawa wa Acacia Walipokuja tuambieni nini tumekipata. Je, tumepata malipo, Je wamesema dhahabu za kiasi gani wamepeleka bure. Mnashangilia maneno matupu hayana mwanzo wala mwisho wala mshikio.Mnaridhika na porojo tu bila kuyaona majibu. Na bado mnalitenga taifa kama kwambammeshatatua matatizo tusonge mbele, Hamuwezi kusonga mbele na kuwaambia Watanzania kama mchezo kwa mambo makubwa kama haya.Tafadharini sana WanaCCM ingawa Raisi ni mwanachama wa CCM. Itendeeni haki nchi na Watanzania ili wawaamini mko na mnalinda maslahi ya nchi hii kwa vitendo kwa kushirikiana na Wapinzani ndio walioziibua hoja zote hizi tunazozizungumzia.Ujumbe na mchango wa Wapinzani Bungeni ni mkubwa sana. Hoja zao ni muhimu sana. Mnawaona Wakosoaji lakini hamuwahusishi moja kwa moja katika mawazo, mipango, na usuluhishi wowote.Wala hamjaheshimu mchango wao itaifa. Kila siku mnawaambia Watanzania ni CCM, na Raisi magufuli tu. Hii ni dhambi na udanganyifu na upotoshaji mkuu tena usiokwisha. Hamjaweza kutulia kukiri makosa, mkakaa chini na wapinzani mkapongezana na kwa pamoja mkajisahihisha kwa manufaa ya nchi. Ni sifa, Kelele, makofi, CCM, hii inachosha na inakatisha tamaa kwa Watanzania wenye elimu, ujuzi , utambuzi na nia njema na nchi hii. Wajinga wengi, wasio na elimu wengi, wasioujua uzito wa mambo haya, na wasio na nia njema na taifa hili, ndio wanaowaunga mikono nyinyi. Na hii ni hatari kubwa kwa Taifa. Wasio na elimu na ufahamu, angalia wanayoyaandika mengi ni utumbo mtupu, na ndio wanaowaunga mikono myinyi. Elimu ndogo. Kosa kila kitu pata elimu itakukomboa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad