VIDEO: Tundu Lissu Ataka Rais Magufuli Asusiwe Kila Mahali na Mataifa Mengine Duniani

Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali.

Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka.

Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu.

Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21. Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu

Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama?
Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa
Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.
Source:Jamii Forums
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Lisu kichwa kinene lakini hamna kitu kati/ka kichwa kile chote yaani kichwa alichonacho ni cha hovyo kabisa. Chuki na mahangaiko ya kuwashawishi wahisani waietenge tanzania pamoja na makelele yake yote hayo akiongozwa na chadema ni ushahidi tosha yakuwa Lisu na genge lake ni maadui wakubwa kwa maisha na maendeleo ya watanzania. Yaani wanapiga kampeni kwa nguvu zao zote kuzuia miradi ya maendeleo isitekelezwe nchini kwa manufaa yanani?Yaani kama kuna mradi wa rail(train) ya kisasa unaendelea kujengwa nchini basi wao wanahangaika kufanya hujuma usifanikiwe? Kama kuna ule mradi wa fly over unaoendelea kujengwa pale Daresalam basi wao wapo vitani kuhakikisha huo mradi unafeli? Kama kuna mradi wa upanuzi wa Bandari kuwa ya kisasa kama mradi uliosainiwa hivi karibuni na wahisani kuipanua bandari ya daresaalam kuwa bora kuliko zote Africa mashariki basi wao wapo mbioni kuhakikisha huu mradi unafeli? Na haya yote nilioandika hapa sio mambo ya kutunga au yakuzua bali ni matamshi yake mwenyewe binafsi Lisu Nnaimani kwa muongozo wa chama chake. Sasa hii kampeni wanaoiendesha kutengwa kwa maghuful na jumuia za kimataifa ni kampeni ya makusudi kabisa ya kuhakikisha Tanzania inabakia kuwa miongoni mwa nchi masikini duniani mpaka kiama yaaani mpaka mwisho wa dunia. Utamkomoa vipi mtu kama maghuful msomi wa pHD ana sifa ya ufanyaji wa kazi uliotukuka katika maisha yake yote bila ya kuikomoa Tanzania? Ni Lisu huyu huyu aliewahi kujiapiza akipinga kufanywa uchunguzi juu ya wizi wa makontena ya mchanga wa dhahabu. Ni Lisu huyu huyu aliongoza kampeni ya kuwaeleza watanzania jinsi gani Edwadi Lowasa alivyooza kwa ufisadi. Sasa leo Lisu amekuwa mshirika mkubwa wa Edwadi Lowasa? Wakati mwengine mtu kama Lisu anapokusanya vyombo vya habari na kuzungumza mambo yake ya hovyo unakaa pembeni na kujiuliza ni kwa dharau gani anayoinyesha juu ya ufahamu wa watanzania juu ya maisha yao? Yaani Lisu anawachukulia watanzania ni watu wenye maono dhaifu na rahisi sana yaani (very cheap people to be brain washed). Kama nilivyo mnukuu yeye mwenyewe binafsi Lisu. Kwamba tanzania hakuna demokrasia na anamfananisha muheshimiwa Magufuli na MObutu, kagame, kabila, Nkuruzima wa burundi? Basi aende tu huko kigali Ruwanda au Bunjumbura Burundi au hata COngo Kinshasa na aitishe waandishi wa habari na aropoke hovyo juu ya viongozi wa nchi hizi kama alivyofanya hapa Tanzania kama atatoka salama? Nadhani umefika wakati watanzania kuacha ushabiki wa kisiasa na kuanza kuwatambua maadui wa maendeleo ya nchi yetu kwani hata Africa kusini ilipiga hatua wakati wazungu waliamua kuijenga ile nchi licha yakuendesha mfumo haramu wa ubaguzi wa watu. Na wakati huo Waafrica wa nchi nyengine licha yakuwa huru viongozi wake waliendelea kusalitiana na kuendeleza migogoro isiokuwa na maana, badala ya kufokasi masuala ya maendeleo wakajikita zaidi kwenye migogoro ya wenywewe kwa wenyewe mingi kati ya hiyo migogoro imepelekea umwagikaji mkubwa wa damu katika baadhi ya nchi. Na hapana shaka Tundu Lisu ni nembo halisi ya baadhi ya viongozi wa Africa waliolipelekea bara la Africa kuwa Dunia ya mapigano na migogoro isioisha.

    ReplyDelete
  2. Hakuna cdm walilo anzisha likafanikiwa so sina wasiwasi na kampeni yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. umenena na lichama lao litafutika karibuni

      Delete
    2. WAPI UKUTA??? PIIIIIPPPPPOOOZZZZ PWAAAAAAA......CHALI, NDEMBE-NDEMBE, KWISHNEY, HAWANA-PA-KUKAMATA-WAMEBAKI-DUH-KWA-ROHO-MBAYA-ZAO...........WAMESHINDWA, WANASUBIRI KULEGEA hahahah HAPA KAZI TU!!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad