VODACOM Tanzania Waichangamkia RED RLX Katika Maonyesho ya Saba Saba
0Udaku SpecialJuly 06, 2017
Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania inashiriki Maonesho ya 41 ya Viwanda na Biashara maarufu kama “Sabasaba” ambapo mamia ya wateja wameoneshwa kufurahishwa na kujiunga na huduma mpya inayojulikana kama “RED RLX” ikiwa ni miongoni mwa huduma nyingi zinatolewa bandani hapo. Huduma hii ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja atumiavyo na lengo ni kuwafanya wateja wa Vodacom waishi bila wasiwasi linapokuja suala la mawasiliano. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja anaponunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.
Mteja wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, atapata huduma ya SOKONI App BURE, taarifa fupi ya M-Pesa BURE pindi anapohitaji na huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja. Ili mteja ajiunge na kunufaika na kifurushi hiki anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi hivi vya RED.
Kifurushi cha Silver
TZS 30,000
600 Dakika (Mitandao Yote)
3GB Data
3,000 SMS
Kifurushi cha Gold
TZS 50,000
1,000 Dakika (Mitandao Yote)
7GB Data
7,000 SMS
Kifurushi cha Platinum
TZS 95,000
2,500 Dakika (Mitandao Yote)
30 Dakika (Kimataifa)
20GB Data
15,000 SMS