WANAMUZIKI wa Kike Maarufu Marekani Waangukia Mapenzi Kwa Mabilionea wa Kiaarabu...Kunani?

Siku za karibuni wanamuziki maarufu wa kimarekani wameangukia kimapenzi kwa Mabilionea wa kiaarabu, Rihanna mwimbaji maarufu huko Marekani ameangukia na penzi kwa bilionea wa kutoka huko Saudh Arabia Hassan Jammel ambaye pia ni mwenyekiti wa kampuni kubwa inayohusika na biashara ya magari ya Toyota huko mashariki ya kati. Mwanamziki mwingine Janet Jackson alifunga ndoa Bilionea Al Mana wa Qatar lakini baada ya kupata mtoto mmoja ndoa hiyo ilivunjika inadaiwa baada ya ndoa hiyo kuvunjika Janet Jackson anategemea kupokea dola milioni 500 kama fidia ya talaka.

Kuna uwezekano hawa wanamuziki wamegundua jinsi ya kuchuma utajiri wa haraka kutoka kwa hawa Mabilionea waarabu kwani Rihanna atakapokwenda kuishi na mume wake huko Saudi Arabia atatakiwa kuvaa mavazi ya kiislam na ni jambo hataliweza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad