Wanaotaka Mh. JPM Aongezewe Muda Wana Hoja, isipokuwa Kuna Sehemu Hawafiki

Wanaotaka Mh. JPM Aongezewe Muda Wana Hoja, isipokuwa Kuna Sehemu Hawafiki
Nikiri tu kwamba nami ni mmoja wa watu ambao naiona dhamira ya dhati ya Mh. Rais wa awamu ya tano katika kulisaidia taifa letu. Kutokana na kauli zake na matendo yake ni wazi Mh. ana kiu ya kuona mabadiliko ya haraka kwa nchi yetu. Mh. anatamani kuona kila mtu anatembea kwenye nyayo zake ili kuifikia kwa haraka dhamira yake njema. (Ingawa kuwa na dhamira njema pia kunategemea sana njia bora za kuifikia dhamira hiyo)

Kitu nachokiona, kuanzia mh. mwenyewe mpaka wafuasi wake yaani sisi tunaoamini katika dhamira yake njema, tunaona kabisa kwa muda wa kikatiba uliopo ni ngumu kuifikia dhamira njema aliyo nayo mh. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia. (

Kutokana na athari za kuona muda ni mdogo, mh. amekuwa akitaka mambo mengi yabadilike kwa haraka kitu ambacho ni ngumu kutokea, matokeo yake ndipo watu wanaona kama mh. anakurupuka kumbe la hasha ni kule kutaka kukimbizana na muda tu.

Kwa upande wa wafuasi nao wameshindwa kabisa kuamini kwamba baada ya muda huu mfupi kuisha atatokea mtu mwingine atakayekuwa na dhamira ya dhati kama ya Mh. JPM. Wengi nikiwepo na mimi tuna wasi wasi pengine mtu ajaye anaweza akaturudisha kule kule tulipotoka, ndipo sasa wanapoona suluisho pekee ni kumuongea muda Mh. JPM (Hapo ndipo tunapoachana na wenzangu walio wengi)

Angalau juzi nimemsikia Mh. Kule Kigoma akitamka kwamba yeye anataka amtengenezee Rais anayemfuata njia ya kuongoza vizuri. Tena akajifananisha na Yohana wa katika Biblia aliyemtayarishia mapito Yesu/Issa bin Mariam. Kumbe Mheshimiwa ana mpango hata wa kutaka kuongezewa muda. Kwa maelezo hayo ina maana wale wanaotaka mh. aongezewe muda wana hoja lakini kuna sehemu moja tu ambayo hawafiki; Tumeshuhudia huko nyuma wakuu wa nchi wakibadilisha badilisha mambo mengi kulingana na wanavyoona inafaa. Mengine yalileta manufaa, na mengine ndio yametufikisha kwenye matatizo haya tuliyo nayo leo.

Sehemu pekee ambayo wenzangu hawataki kufika ni kwenye marekebisho ya katiba. Baba yetu Magufuli chonde chonde tuachie katiba mpya baba. Na katiba hiyo si nyingine ni ile ya Mh. Warioba. Kwa kutupa/kutuachia katiba safi, si tu itakupa heshima na kudhihirisha wazi dhamira yako njema, bali itafanya hata anayekufuatia kutokuturudisha kule kule tulipotoka. Lakini pia itatupa meno meno na sisi kuwashughulikia wawakilishi wetu wa hovyo. Kwa katiba ile hata hawa wawakilishi wanaosadikikika kuwa wachochezi, tutawaondoa wenyewe maana tutakuwa tumepewa meno ya kuwaondoa.

Nakaribisha majadiliano yenye afya.

By Dmketo
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa jinsi hii nchi ilipokuwa imefikishwa na mafisadi na wapiga dili, bila 'UDIKTETA' hii nchi haitaenda kabisa..........

    ReplyDelete
    Replies
    1. umenena lazima kukomaa nao

      Delete
  2. Udikteta ni maoni ya mtu binafsi.Huwezi kuliendesha taifa kwa maono binafsi.lazima raidi afuate misingi ys nchi.Bila katiba nchi haina meno. Atajifunga mwenyewe. Maoni yake binafsi si maoni ya watanzania na hili ni tatizo.kuna mambo mengi anafanya si sahihi sababu hata yeye hafuati
    sheria.Kiongozi yeyote ambaye anavunja sheria za nchi na kuzidharau hata akiwa na nia njema ajue anavunja sheria za nchi pia. Unapoona wanasheria wanaungana ujue kuna tatizo. Na hata wanaomuunga mkono hata wao hawajui sheria. Huenda hsna dhamira mbaya, bali skiwa msikivu, akiwa na washauri wazuri watamshauri.ksma wanashindwa ujue, wanameogopa, na kama wanameogopa basi neno dictator ndo linapoingia apende asipende.muda utafikia sheria itamfikia atapoteza kila chema alichokitarajia.Na inaenda huko. Kwa waliodhujaa watamsihi, dhaifu watampaka mafuta wapate chao. Cheo, au ahadi fulani zitimizwe ingawa ni haki zao itabifi wamwinamie kama alivyofanya nfugu Zitto. Kamwinsmia. Ajue hata yeye anajipunguzia ushujaa wske pia. Anataka kuwa raidi unaona waxi hana msimamo kamili. Anatofautiana na ndugu Kafulila. Kafulils kamshukuru zaidi lakini kaenda mbali zaidi na kumwambia wazi, ccm imemwibia kura zake. Leo anampongeza lakini naye ni mhusika kwa kupokonywa kwa kiti cha Kafulila. Hii ni dhurma ya haki ya binadamu fulani na kumfaididha meingine. Na hii ni moja wapo tunaipigs vita.Bila Kafulila, Mnyika, hii Iptl na escrow hazingekuwa zimeibuliwa. Na wapinzani hasa chadema, ambao sasa wanadharalishwa ni wso tu ndio waliopigania haki na di ccm.leo ccm inachukua sifa si yao.wote wsliohusika, watuhumiwa wa haya yote ni viongoxi wakuu wote wa Chama cha ccm. Ndio kwa miaka yote hii wamebebana na kudhurumu nchi na kujigawia wao, watoto zao, na marafiki. Leo bado wanatoa amri serikalini. Ni ujinga gani watanzania tunao kwa kutokuliona hili.mwizi wa kuku mitaani mnampiga tofali mpaka anakufa. Mwizi mwenye njaa anashindwa kununua mnamfunga miaka kumi. Lakini nawashangaeni wsnaccm eote kumruhudu raisi kutowachukulia hatua viongozi hudika wa juu maraisi na wengine na mnampigilia makofi na mnafurahia kuwaona wanasheria wadai haki kama ndugu Lisu kukamatwa wakidai haki zitendeke, je tumelogwa?.tukiambiwa didi ni wajinga kwa nini tunakadirika.mnawaona viongozi wanatumia vyeo vyao vibaya, wameshusha elimu, lakini angalieni watoto wao wapo nje kwa elimu za gharama za juu mnachofurahia ni nini. Hampendi elimu sawa kwa wote.mnaona viwanda vinapelekwa kwao, mikoa mingi mnawachagua hawa viongozi mnaibiwa tu, hamkadiriki.viwanda sita au nane sehemu moja, nenda kibiti hata elimu shida. Mnamtafuta mchawi. Na mnamjua mchawi wenu, halafu mnashangaa wananchi wanapochukua dheria mikononi. Mnawabambikizia kesi haziendani na ukweli. Lini watanzania mtaelimika mufunguke.ebu fungukeni, muuone ukweli badala ya kurundikana kwenye mikutano ya mapokezi yasiyo na ukwreli halisia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. katunge kitabu maana unatutia uvivu kusoma maana hata maneno mengine hayasomeki unaonekana ulivyo kilaza

      Delete
  3. Nakubaliana 100% na mtoa hoja. Ameongea vizuri sana kwa maslahi ya Tanzania, bila kuweka itikadi za uchama. Hapa bwana mkubwa atupe tu Katiba ya Warioba tumalize mchezo.
    Asante sana mtoa hoja.

    ReplyDelete
  4. Binafsi namkubali Maghuful tena sana kiasi kwamba nashindwa kuamini mpaka hivi sasa kwamba Maghuful ni Mtanzania? Watanzania wengi ni wingi wa maneno na usomi ni njia moja ya kujipatia kipato kwa njia za ubadhirifu kutokana na nyadhifa watazozikwaa. Labda kwa kuwa nimekuwa nikiishi nje kwa miaka mingi lakini kila nikizeleta kumbukumbu zangu nakumbuka mikiwa mdogo kama mtu akipata madaraka serikalini kama hakuiba haraka na kutengeneza maisha anaonekana mpumbavu wa hali ya juu. Nadhani na ni hizi fikra potofu ndizo zikazoeleka kuwa mfumo halali wa maisha ya watanzania. Nilishuhudia kesi moja katika nyingi hapa Marekani ya mtoto kwenda kumshitaki babayake mzazi kwa kosa la kutokulipa kodi kwenye kituo cha kuuza mafuta (gas station) au sheli kama mnavyoita huko nyumbani. Mtoto aligundua mchezo mchafu wa ukwepaji kodi wa baba ake baada ya kuajiriwa na mzee wake kama meneja. Maisha yetu Tanzania yamejaa udanganyifu mno licha ya kujifanya ni watu wa dini. Kwa upande na ufahamu wangu watanzania hawapaswi kumtizama Magufuli kama Raisi au mwanasiasa tu bali wanatakiwa kumtizama Magufuli kama mwalimu muadilifu anaewapeleka katika mfumo sahihi wa maisha. Elimu anayoitoa Maghuful kwa watanzania katika mambo mbali mbali yaani anafanya kazi ya kuwafunua macho hasa. Hiyo elimu ya namna hiyo ilihitaji foreign experts yaani wataalamu wa nje na si mmoja ni zaidi milion moja kutokana na idadi ya watanzania na geographical nature of our country. Hakuna short cut katika maisha na hilo ni agizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mmiliki wa kila kitu. Na hakika kwakua ni agizo la Mungu jamii itakayoamua kuishi katika misingi ya ulaghai na ubadhirifu basi inawezekana kwa muda mfupi wakajisikia mambo poa kabisa lakini hakika jamii hiyo haitokuwa salama na mateso ya dunia kwa muda mrefu hasa ufakara. Na hakika adhabu ya M/Mungu kwa wahusika wa rushwa na dhluma ni kubwa mno tena huanzia hapa hapa duniani amini au usiamini kwa wenye kuzitambua Kudra za Mungu adhabu kwa wale walizoea kuishi kwa njia za dhluma basi wamwangalie Magufuli na vibano na aibu wanazozipata wahusika wa makosa ya Ufisadi Tanzania. Siami ni nguvu za Maghuful tu aliekulia ndani CCM hafla ajekuwa ndie kiongozi anaeongoza vita vya Ufisadi kwa asilimia 100% hapana shaka ni mkono wa Mungu. Na kama watanzania watamsikiliza na kumuelewa Magufuli basi hawapo mbali na Neema tena neema kubwa sana. Lakini licha ya karama zote hizo za Maghuful siafiki wazo la kumshawishi au kumfanyia kampeni kuongoza nchi zidi ya utaratibu tuliojiwekea. Sidhani hata kama yeye mwenyewe Maghuful anakubaliana na wazo hilo ni mtu smart sana tofauti na watu wanavyomuangalia kijujuu labda Ngosha tu yule bwege fulani hapana yule muheshimiwa Magufuli Mungu kampa fungu zuri sana la kuelewa mambo na Mungu amzidishie Amin. La msingi watanzania tumpe sapoti kubwa bila ya uoga wa aina yeyote kwa kuwa anasimamia haki basi baada ya muda wake kwisha wa kulitumikia taifa kama raisi na M/Mungu atatupa sapota kubwa sana kwa kuwa watu wa kupinga maovu na kusimamia haki na hapana shaka kwa uwezo na upendo M/Mungu atatujalia kiongozi bora zaidi kuliko wa awali. La msingi kama watanzania ni kutambua na kushukuru neema za M/Mungu kwani Maghuful ni miongoni mwa neema hizo kwa tatizo lilokuwa nalo Tanzania katika kumpata kiongozi atakaejali vilio vya wanyonge basi ujio wa uongozi Maghuful hapana shaka vilio vimefika kwa Mmiliki wa kila kitu ambae ni Mungu Muweza wa kila kitu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad