ZITTO Kabwe Awaamshia DUDE Chadema.......

KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, katika kile kilichoonekana kuwapa kijembe Chadema, akisema kutaka nchi kunyimwa misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia inapaswa kupiganwa ndani.

Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.

“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia,” aliandika Zitto.

Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakipingana naye.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unajikoroga mwenyewe.nilimpeda mamako, nilimfuatilia kisiasa, alikuwa mwanamke si mwoga. Alikupa wosua, unausahau sababu ya kutafuta ufalme. Mama anajua. Fikiri, tulia usipopata jibu moyoni hata ukiwa na akili hutaendelea. You are not sincere. Hii itakuangusha. Dhamira huna, kama unayo, unapokiuka itakusonga. Lakini huwezi kuikandamiza muda wote, itakutafuna mzima.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad