ACT- Wazalendo Wamtolea Tamko Rais Magufuli

Chama cha *ACT Wazalendo* kimeshtushwa na kauli (amri) ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli aliyoitoa hivi karibuni akiwa Mkoani Tanga ya kutaka Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mazingara, Kata ya Mkata, Wilayani Handeni , katika Mkoa wa Tanga ahamishwe katika kituo hicho mara moja.

Hatua hiyo ni baada ya malalamiko ya mkuu wa wilaya ya Handeni , ndugu Godwin Gondwe kuwa kesi zote kati ya wakulima na wafugaji katika mahakama hiyo wanashinda wafugaji, na hivyo kumtuhumu hakimu huyo, aliyetajwa kwa jina moja la Laizer kuwa anapendelea wafuagaji.

*ACT Wazalendo* tunalaani kauli hii ya Rais kwa kuwa inakiuka misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara 107B ambayo inaipa Mahakama Haki na Uhuru wa kufanya kazi yake bila kuingiliwa wala kubughudhiwa na mihimili mingine. Katiba inaainisha mgawanyo wa Madaraka baina ya Serikali, Mahakama na Bunge.

Kitendo cha Ndugu Rais kutaka Hakimu wa Mahakama achukuliwe hatua kwa kuhamishwa ni kuuingilia Mhimili wa Mahakama ambao katiba na misingi ya utawala bora inahitaji mhimili huo pamoja na wanaohudumu wawe huru na kufanya kazi zao bila ya shinikizo la mtu yeyote iwe la kisiasa au kijamii.

Sisi *ACT Wazalendo* tunaamini kuwa hata kama tuhuma dhidi ya Hakimu mhusika ni za kweli, na kuwa ipo haja ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake, basi lazima utaratibu wa hatua hizo za kinidhamu kwa Hakimu huyo ufuatwe, kwa kuchunguzwa kwanza, kupata ushahidi na akikutwa na hatia basi achukuliwe hatua na mamlaka yake ya nidhamu, ambayo ni Tume ya utumishi wa Mahakama. Hatuamini kama hakimu anayedaiwa kupendelea katika kutoa hukumu anapaswa kuhamishwa tu.

Ni wazi kauli hii ya Rais inalenga kuwatia hofu Majaji na Mahakimu wengine. Na utekelezaji wake utaiaminisha jamii kuwa hatima za Majaji na Mahakimu katika kazi zao zipo mikononi mwa Rais na sio utaratibu wa Sheria uliowekwa. Amri hii ni batili, ni kinyume cha Katiba, na ikitekelezwa ni uvunjifu wa Katiba ya Nchi!

Katika jambo hili, *ACT Wazalendo* tunamtaka Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma ajitokeze hadharani kukemea amri za namna hii zinazoudogosha mhimili wa mahakama, atoe kauli ya kuwahakikishia Mahakimu na Majaji kuwa usalama wa majukumu yao (security for tenure) unalindwa na utaendelea kulindwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi. Na kuwa kama yapo malalmiko juu ya hakimu Laizer basi utaratibu ufuatwe.

*ACT Wazalendo* pia inamsihi Rais kumchukulia hatua za kiutawala Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bwana Godwin Gondwe Kwa kumwingiza Rais kwenye mgogoro wa kikatiba usio wa lazima. Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa vikao vya ngazi za chini vya michakato ya kutazama maadili ya mahakimu na anajua taratibu za kufuata. Alichofanya Mkuu wa Wilaya ni kitendo kinachopaswa kukemewa kwa hatua kali kuchukuliwa dhidi yake ikiwemo kumwajibisha ili iwe fundisho kwa Wakuu wa Wilaya wengine wanaoshindwa kufanya kazi zao.

Mwisho, tunavitaka vyama vya mawakili vya Tanganyika na Zanzibar na taasisi nyengine zenye kupigania utawala wa Katiba na Sheria nchini kujitokeza na kulaani kauli ya Rais na kumshinikiza Rais au kupitia waziri wake wa Katiba kuwaomba radhi watanzania kwa jaribio hili la kutaka kuvunja misingi ya katiba waliyoapa kuilinda.

Thomas E. Msasa
Mwenyekiti- Kamati ya Sheria na Katiba
ACT Wazalendo
Agosti 09, 2017

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tOMASI mSASA... uNAHITAJI KUPIGWA mSASA. mAGUFULI AMESHAPIMA HAYA YOTE YA KUFIKIA HATUA YA MWISHO ITAKUJA KUWA HIYO ILA MUDA UTAKUWA NI MREFU SANA MPAKA KUFIKA HAPO. NA HATIMA YAKE ITAKUWA HII ILIYO SHAURIWA LEO. WHY WASTE TIME. ETI.... AMKA HII HAIHITAJI MSASA HATA KAMA UNAKUTU ... NI UWAHI KULALA NA UKIAMKA JIBU NI HILI HILI .

    ReplyDelete
    Replies
    1. hovyooo watu wanaongea mambo ya maana we unaleta umbumbumbu wako, unajua kuwaste time maana yake nini?

      Delete
    2. Unauliza jibu au swali?

      Delete
  2. Mnashangaa tena. Jipi jipya. Wengi mmemshangilia kwa muda mwingi sana. Akitumia tumbua tumbua na mara nyingi hii tumbua tumbua ambayo mara nyingi haifuati sheria.anatumbua huyu kumuacha mwingine bila kujua kanuni gani anaifuata.wengine huwaacha kutokana na ukaribu nao.kafanya hivi kwa wanachadema toka aingie madarakani.wengi hawasikilizi na kuwasaidia waombapo maendeleo kwenye majombo yao, kisa wapinzani. Ksma Manji anavyowakataa chadema kuwa wawakilishi wake. Raisi amezidi kuligawa taifa kibendera, ccm au chadema. Sasa nashangaa ACT kuchukua muda mwingi bils kuliona hili.ndugu Magufuli toka aingi madarakani kazi yake imekuwa kuvunja vyama upinzani vyote na kuimarisha ccm. Kuadhibu watu apendavyo. Na wakuu wa mikoa ksma Makonda wasio na elimu mbadala wakiiga kila alifanyalo. Kuadhibu watu wapendavyo sababu anawakingia kifua. Imekuwa viongozi wa ccm wanamwogopa kufanya kazi zso na kufanya makosa pia. Hawajiamini , wanatetea vyeo vyao. Na hii ni hatari kubwa.

    ReplyDelete
  3. Kwani huyo zito si alilani na kujiapiza akimuonya Maghuful aache kabisa kuwapiga mkwara watu makinikia ya mchanga wa dhahabu. Zito wakati mwengine hana jipya anatafuta kiki tu.

    ReplyDelete
  4. Kwni majaji ni malaika? Raisi ni mtu mwenye utajiri wa kinteljensia sasa je ikajakugundulika huyo jaji anamiliki mbuga yake iliyojaa ng'ombe wa ruswa yeye zito yupo tayari kujiuzulu na siasa? Katika suala la makinikia Zito alipwiyanga lakini la kushangaza akashindwa kuomba radhi kwa watanzania leo tena anamwingilia muheshiwa raisi katika maamuzi kabla hata ya kuujua undani. Tatizo la watanzania awe mwanasiasa,michezo, kila mtu anajifanya anajua lakini hakuna cha maana kinachoonekana kutoka kwa hao wanaojifanya wanajua zaidi ya kelele tu.

    ReplyDelete
  5. huyu ni msanii mwingine wa msasa na anajiita Msasa Tomasi..wa wapi huyu?? eti na maombi pia katoa kwa kina na vile wale wa Tanganyika na wa kule visiwani eti sijui wafanye nini??... Ndio wale wale..!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad