Agnesi Masogange Akutwa na Kesi ya Kujibu Atakiwa Kujitetea


Agnesi Masogange Akutwa na Kesi ya Kujibu Atakiwa Kujitetea
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ ana kesi ya kujibu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya, hivyo anapaswa kujitetea.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka, ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na ana haki ya kujitetea.

Baada ya kuelezwa hayo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi 3.

Kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017 ambapo Agnes Masogange ataanza kujitetea.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad