Alichojibu Polepole Baada ya Kuambiwa viatu vya Nape Vinampwaya

Alichojibu Polepole Baada ya Kuambiwa viatu vya Nape Vinampwaya
Kupitia kwenye account yake ya twitter Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole ametoa majibu kwa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akimwambia kuwa hatokuwa tena Mbunge baada ya Awamu hii.

Hatua hiyo ya Polepole imekuja baada ya kuambiwa na Mbunge Msigwa kuwa viatu vya Nape havimtoshi kupitia twitter ambapo aliandika; "Kitendo cha Msukuma kumkumbuka Nape , ni ujumbe tosha Kuwa Viatu vya Nape vinampwaya POLEPOLE!"


MsigwaPeter
"Kitendo cha Msukuma kumkumbuka Nape , ni ujumbe tosha Kuwa Viatu vya Nape vinampwaya POLEPOLE!"


Baada ya ujumbe huo naye Polepole kupitia twitter aliandika; "Kitu kimoja nakuahidi, hii ni term yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona mchungaji anajichanganya na mbuzi."

Humphrey Polepole @hpolepole
"Kitu kimoja nakuahidi, hii ni term yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona mchungaji anajichanganya na mbuzi"


Je Kwa Unavyoona ni Kweli Viatu Vya Nape Vinampwaya?
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Polepole bado nimtoto akiliyakeinakua kwakuangaliajua

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad