Alikiba Na Diamond Waendelea Kuchuana Vikali Views Youtube.....Kiba Aendelea Kuongoza

Alikiba Na Diamond Waendelea Kuchuana Vikali Views Youtube.....
Wimbo mpya wa Alikiba ‘Seduce Me’ ulioachiwa Ijumaa hii unaendelea kutrend kupitia mtandao wa video wa YouTube huku nafasi ya pili ukifuatiwa na wimbo mpya wa WCB, Zilipendwa.

Video ya muimbaji huyo wa RockStar400 mpaka sasa ina views 1,225,781 ikiwa ni video ya kwanza kuachiwa kabla ya WCB iliyoachiwa jioni yake.

Video ya WCB ‘Zilipendwa’ mpaka sasa ina views 736,323  ikiwa ina saa 12 toka iachiwe kupitia YouTube.

Kitendo cha WCB kuachia video ya wimbo huo muda mchache baada ya Alikiba kuachia Seduce Me, kumewafanya mashabiki wa wasanii hao kushindanisha project hizo mbili ambazo bado zinashindana kupitia mtandao wa YouTube.


Wawili hao kila mmoja anaonyesha bado ana hasira na mwenzake kwani kila mmoja anamtishia mwenzake ataachia ngoma nyingine.

Alikiba anadaiwa kutweet kwamba wimbo ‘Secude Me’ alikuwa anatesh mitando huku akidai ngoma kamili inakuja.

Kwa upande wa Diamond naye kupitia meneja wake Sallam amedai kwamba baada ya ‘Zilipendwa’ wataachia wimbo mpya ambao Diamond ameshirikiana na msanii mkubwa wa kimataifa.

 Itazame  ZILIPENDWA  ya  Diamond
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kiba hana majivuno tabia nzuri of course ukiwa na moyo msafi kika mtu atakupenda lakini mwenzangu huyu aliekataa damu yake kumdhalilisha mwanamke hivo kweli utaendelea kweli haya tukuna macho eeh ila kiba bwana seduce kiboko yao umewatoa jasho hadi wameunga kwaya aisee

    ReplyDelete
  2. Huna jipya ww sisi tunauliza ipi ngoma kali unaleta habari za kutelekeza watoto nenda zako kule pumbav

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad