Aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ''ametorokea ngambo'' kulingana na duru wakati ambapo anatarajiwa kuhusu kesi inayomkabili ya uzembe.
Duru katika chama chake zinasema kuwa alichukua uamuzi huo wa kuondoka kwa ghafla, muda mfupi kabla ya kuwasili mbele ya mahakama ya juu kuhusu mashtaka ya kuzembea.
Mawakili wake wameambia mahakama kwamba alishindwa kuhudhuria kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Lakini aliposhindwa kuwasili , mahakama ilitoa agizo la kumkamata na kufutilia mbali dhamana yake.
Majaji pia waliahirisha uamuzi huo hadi Septemba 27.
Bi Yingluck amekana kufanya makosa yoyote katika mradi huo ambao uliigharimu Thailand mabilioni ya madola.
Iwapo atapatikana na hatia baada ya makosa hayo ya miaka miwili, anaweza kufungwa jela hadi miaka 10 na kupigwa marufuku katika siasa.
Duru katika chama cha bi Yingluck zimeambia Reuters kwamba aliondoka Thailand lakini hakutoa maelezo ya kule aliko.