"Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito, serikali inaamini tuna wajumbe makini huku ndani wasioyumbishwa na vishawishi vya muda na vishawishi vya mpito, tunataka viongozi wanaongozwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo tunataka viongozi bora wa TFF wenye hali, moyo, uelewa, weledi na uadilifu unaotakiwa kupeleka soka letu mbele" alisema Mwakyembe
Aidha Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa yoyote ambaye anaona amegombea nafasi yoyote ndani ya TFF kwa lengo la kujipatia fedha au kutajirika basi anapaswa kutambua kuwa amepotea njia.
Msikilize hapa Mwakyembe akifunguka zaidi.
Mwakyembe amesema rais na wajumbe watakaopatikana leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakishahau haki ya waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.