Askofu Bagonza Akosoa Kauli ya 'Aliyepewa Mimba Asirudi Shule', Ahoji Makosa Serikalini Yangekuwa Mimba, Wangekuwa na Ngapi?

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe Dr. Benson Bagonza, amewapasha viongozi wote serikalini wanaoshabikia wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo,amesema "kama hawa viongozi wote wangekuwa kila kosa wanalofanya ni mimba tungezalisha mimba ngapi?

Akaendelea Mungu hua anatoa nafasi ya pili ili mtu atengeneze lkn wao viongoz wamejipa mamlaka ya kuhukumu hao hao ndo wanasema mwanafunz akipata mimba hakuna kusoma alisema huku akishangiliwa na wananchi na kujiamini bila wasiwasi wowote, huyu naona ndo Askofu wa kwanza kuanza kukosoa serikali hii kwa mambo ya ovyo ovyo inayofanya,

 Askofu Bangoza, amekuwa akiikosoa Serikali bila woga pale inapokosea.

VIDEO:

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wape hao. Makanisa mengine hayatoi ukweli. Wanatumika na siasa badala ya kutetea Jamii. Na viongozi wanatumia makanisa kujificha huko. wanakwenda kanisani kutumia hekalu la Mungu kwa manufaa yao. Makanisa yanatumiwa wakati wakura. Lakini makanisa yangemsimamia maskini na kutetea haki za maskini ambazo ndizo kazi zao, hawa viongozi kamwe wasingeonyesha nyuso zao huko. Mungu anasema tenda haki, simamia haki, viongozi wengi tunawajua wezi, wametuibia, bado wanakwenda kanisani na kutoa michango ila tu waungwe mikono. Na waengi wafuasi wa dini mbalimbali, wangekuwa wacha Mungu kiukweli, sidhani kama Tanzania ingeyumba ilivyoyumba kwa miaka 15.Wengi wanaojiita waumini, ndio wanaowatetea viongozi haramu, ingawa wanajua hawa viongozi ndio waliotusababishia haya, na wanaotuletea umaskini nchini kwa kuisaini mikataba mibovu kuwapa wazingu na ndugu zao huku maskini na nchi ikianguka vibaya. Sifahamu kama dini zinafundisha pia kutokufikiri, kutokudadisi na kusema mungu atawapeleka motoni badala ya kujipa nguvu na kuwapinga na kutowapigia kura waongo.
    Nakusifu baba askofu msema kweli wa Mungu. si wale waliopokea migawo. Labda na wakuu wa dini wengine watafuata.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad