Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Aristica Cioaba ameanza majigambo yake kwa kudai atahakikisha timu yake inaichakaza Simba katika mechi ijayo ili iweze kujikusanyia alama nyingi katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara
Kocha Cioaba amesema hayo baada ya kuona namna ya uchezaji wa wapinzani wao walicheza siku ya Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting FC na kutoka na ushindi wa mabao 7-0.
"Simba ni moja ya timu nzuri wanacheza mpira mzuri, na sasa wasubiri kitakachotokea kwenye mchezo huo. Timu yangu (Azam FC) malengo yake hivi sasa tumejipanga katika kila mchezo ni kuwa makini na kukusanya alama nyingi kadiri iwezekanavyo katika mashindano haya ya Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Cioaba.
Timu ya Azam inatarajiwa kushuka dimbani Septemba 2 mwaka huu dhidi ya Simba SC huku ikiwakosa wachezaji wake wawili ambao ni nahodha Himid Mao 'Ninja' pamoja na kipa Mwadini Ally ambao watakuwa katika timu ya Taifa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana siku hiyo.