Baada ya Raila Odinga Kulalamika Anaibiwa Kura, Tume ya Uchaguzi Kenya Yaamua Kufatilia Ukweli....

Baada ya Raila Odinga Kulalamika Anaibiwa Kura, Tume ya Uchaguzi Kenya Yaamua Kufatilia Ukweli....
Tume  huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imetoa tamko kufuatilia malalamiko yanayotolewa na mgombea Urais Raila Odinga wa National Super Alliance (NASA), kuwa matokeo hayo yanatangazwa bila kufuata utaratibu wa kutoa Fomu 34A.

 Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati ameeleza kuwa tume yake inafuatilia madai yanayotolewa na Odinga kuhusu mfumo unaotumika kutoa matokeo ya Urais, pia wameagiza kuletewa fomu zote namba 34A na 34B kutoka kaunti zote ili kulinganisha matokeo yanayotoka.

Pia Chebukati ameeleza kuwa tume hiyo ina siku 7 za kutangaza matokea na leo ni siku ya 2 , bado wanasiku 5 za kutangaza matokea kwa hiyo kila kitu kitaenda vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad