Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi amesema aliyekuwa Waziri wa Nishati na Mdini,William Ngeleja kupitia pesa alizozirudisha hivi karibuni ni wazi kuwa ni mtuhumiwa ambaye anaweza kutaja wenzake wote.
“Kumkamata Mhe. Lissu hakuwezi kufanya ndege yetu iliyokamatwa kurejeshwa nchini kwani yeye amewasaidia watanzania kufahamu nini kinachoendelea. Sisi ni upinzani tunaopinga na kutoa njia elekezi, katika barua yetu tumemtaka IGP amkamate Ngeleja na wenzake watoe bilioni 307 zetu na Lugumi bilioni 38 kisha wakalipie ndege iliyokamkatwa kwa pesa ya bilioni 87 ili iendelee na kazi lakini siyo kusingizia upinzani kwamba wanapotosha au wanafanya uchochezi,” amesea Mwenyekiti huyo.
“Tufanye kama jinsi ilivyokuwa kwenye Biblia kwamba yule mfungwa Baraba aliachiwa huru kisha Yesu akasulubiwa, basi na Lissu tumuachilie kwani hana kosa zaidi ya kuzungumza ukweli na Ngeleja aliyekiri hadharani kwa kurudisha pesa za wizi awekwe ndani na asaidiane na jeshi la polisi”.