Bill Nasi Aeleza Sababu ya Kutotoa Nyimbo za Mapenzi

Bill Nasi Aeleza Sababu ya Kutotoa Nyimbo za Mapenzi
Msanii wa muziki Bongo, Bill Nass ameleeza sababu ya kutotoa nyimbo zenye maudhui ya mapenzi.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sina Jambo’, ameiambia Live Entertainment ya Azam Tv kuwa anafanya hivyo ili kuleta utofauti katika muziki wake.

“Mimi pia naangalia utofauti huo kwa sababu tukiwa wote 10 tunaimba nyimbo za aina moja au topic moja si rahisi mtu kusikiliza nyimbo zote hatapata choice za hapo hapo” amesema na kuongeza.

“Ninavyoona mimi kuchagua lazima uwe tofauti, wote mkifanana hamuwezi kufika sehemu, mwezio akienda hivi, wewe unaenda hivi unajaibu kutafuta utofauti ili uweze kupata fan base tofauti,” amesisitiza.

Mara ya mwisho Bill Nass kutoa wimbo wa mapenzi ulikuwa ‘Raha’ ambao alimshirikisha Nazizi kutoka nchini Kenya pamoja na TID, pia wimbo huo ndio ulimtoa kimuziki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad