Chadema Yapokea Kwa Masikitiko Taarifa ya Kuungua Kwa Ofisi ya Mawakili

Chadema Yapokea Kwa Masikitiko Taarifa ya Kuungua Kwa Ofisi ya Mawakili
Dar es Salaam.Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko taarifa za kuvamiwa kwa  ofisi za Kampuni ya Mawakili wa Kujitegemea ya IMMMA ya Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano na Mambo ya Nje John Mrema ilisema kwamba Chadema  inafahamu kuwa kwa mujibu wa Mikataba ya Kimataifa Mawakili wana haki ya kufanya kazi zao kwa uhuru na faragha wakati wa kutoa huduma zao kwa wateja wao na wananchi kwa ujumla. Ikumbukwe pia kuwa kwa  mujibu wa Sheria ya Mawakili (The Advocates Act) Mawakili ni Maaofisa wa Mahakama ambao huisaidia Mahakama katika kutenda haki.

‘’Kwetu Chadema tunaona kuwa hili ni shambulio dhidi ya Mahakama kwani maafisa wake wameshambuliwa’’ imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa hiyo uvamizi wa ofisi za Mawakili unalenga kukiuka misingi ya ya Sheria na Mikataba ya Kimataifa inayolinda haki za Mawakili . Chama kinapenda kutoa rai kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wahusika wanapelekwa kwenye vyombo vya Sheria ili Sheria zichukue mkondo wake.

Aidha kitendo hiki kimefanywa na watu waoga wanaodhani kuwa kwa kufanya hivyo kutawafanya Mawakili wawe na hofu nchini na washindwe kutimiza wajibu wao, hivyo basi CHADEMA kinawatia moyo Mawakili wote nchini wasikubali kuingia hofu wala woga kutokana na tukio hili bali waendelee kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria.

Mwananchi:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad