Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako.
Rais wa China Xijinping amemtaka rais Donald Trump kuchunga mtamshi na vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi ,chombo cha habari cha kiserikali kimeripoti.
Rais Trump na Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche za maneno huku rais rais huyo wa Marekani akionya kuikabili kivita vikali Korea Kaskazini.
Lakini China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini ametaka pande zote mbili kuwa na uvumilivu.
Rais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho
Rais Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamekuwa wakirushiana cheche za vitisho
Taarifa ya ikulu ya Whitehouse imesema kuwa Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inafaa kusitisha uchokozi na tabia mbaya.
Hofu kubwa inayoendelea kutanda kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini ilizidi baada ya taifa hilo kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako