Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange amesema anatamani kungekuwa na sheria inayowabana wanaume ambao wana tabia ya kukataa ujauzito, kwani kitendo hicho hakifai kwenye jamii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Dayna amesema yeye kama miongoni mwa wanawake ambao wanalea mtoto bila msaada wa mzazi mwenza, anaumizwa na tabia hiyo, hivyo anatamani nchi ingeweka sheria kuwabana watu hao.
Akielezea suala hilo kwa hisia hadi machozi yakianza kumtoka, Dayna alisema "hicho kitu kinaniumiza sana, yani natamani kungekuwa na sheria fulani ikitokea tu umekataa tu mimba, bado hadi mtoto anazaliwa unakataa, upewe adhabu ambayo itakuumiza sana maishani mwako".
Dayna ambaye ana mtoto ambaye yuko darasa la 5 sasa na anapambana mwenyewe kuhakikisha anapata mahitaji yote, amesema yeye alipitia wakati mgumu mpaka alikuwa na chuki juu ya mzazi mwenzake, hali ambayo ilimfanya afunge na kumuomba Mungu ili aweze kuondoa roho ya chuki dhidi ya mzazi mwenzake, mpaka sasa wako sawa kimaelewano.
DAYNA NYANGE: Natamani Kungekua na Sheria Inayowabana Wanaume Wanaokataa Mimba
1
August 31, 2017
Tags
Si swali la sheria tu, sheria inavipengere vyake Pia, siku hizi baba asingiziwi mtoto DNA inausika baba akikataa, kwani pengine baba amejua hapa nimebambikiwa, DNA ikikubali baba hana jinsi ya kukakata ni jukumu lake pia
ReplyDelete