Dayna Nyange:Sijawahi Kutoka Kimapenzi na Star Yoyote wa Bongo

Dayna Nyange:Sijawahi Kutoka Kimapenzi na Star Yoyote wa Bongo
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hajawahi kutoka kimapenzi na star yeyote Bongo na hataki kufanya hivyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’, amesema sababu ya maamuzi yake ni kufanya mahusiano yake kuwa binafsi zaidi.

“No siyo star, sijawahi date na star na sitamani ku-date na star na sitaki ku-date na star na sito-date na star,” Dayna.

Pia msani huyo ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano lakini anapenda kuyafanya siri sana kiasi kwamba hata mama yake mzazi hajui.

“Naogopa atakasirika ataniacha kwa sababu nampenda, ni mtu ambaye ana wivu, nilishawahi kusema sina mahusiano akachukia nikaoni ok, isiwe shida nipo kwenye mahusiano lakini hayatambuliki kokote hata mama hamjui,” amesema Dayna

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad