Dereva Aliyesababisha Ajari ya Treni Morogoro Akutwa na Mashtaka 30

Dereva Aliyesababisha Ajari ya Treni Morogoro Akutwa na Mashtaka 30
Dereva wa daladala aliyesababisha ajali iliyoua wanafunzi watatu na abiria wengine 27 kujeruhiwa mkoani Morogoro amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka 30, likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kugonga treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Charles Petro ambaye alipata majeraha kwenye ajali hiyo amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Joyce Mkoi.

Wakili wa Serikali, Caristus Kapinga amedai Agosti 24 asubuhi, kwenye makutano ya reli na barabara eneo la Tanesco, Manispaa ya Morogoro mshtakiwa alitenda makosa hayo.

Kapinga amedai kwa makusudi, huku akijua kufanya hivyo ni kosa mshtakiwa aliendesha gari aina ya Nissan kwa uzembe na kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Kutokana na ajali hiyo, wanafunzi watatu walifariki dunia na abiria 30 walijeruhiwa wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizoko Kihonda na Msamvu katika Manispaa ya Morogoro.

 Mshtakiwa amekana mashtaka yote na  hakimu ameahirisha kesi Hadi Septemba 13 itakapotajwa.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi haujakamilika. Mshtakiwa amepelekwa  rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya  Sh10 milioni na mwingine kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad