Diamond, Kiba na Dimpoz Mtafaruku Wenu Ulipofika sio Burudani Tena, ni Fedheha Kwa Macho na Masikio ya Wengi

Dear Diamond, Ali Kiba na Ommy Dimpoz mtafaruku wenu ulipofika sio entertainment tena, ni fedheha kwa macho na masikio ya wengi. Imetosha sasa, msiendelee. .

Tafadhali, zipelekeni hasira zenu kwenye kufanya muziki mzuri na kuipeleka Tanzania mbele zaidi. Bifu hii isije kusababisha madhara ambayo yangeweza kuzuilika kama busara, uvumilivu na hekima zikitumika. .

Wazazi, watoto, wapenzi wasiingizwe kwenye mgogoro huu, katu hawahusiki. Ali na Diamond, mnajua mlivyo na nguvu kwenye muziki wetu, tangu bifu yenu ianze mnazungumziwa ninyi tu, wasanii wengine wala hawazungumziwi, hiyo ni mbaya kwa industry.

Bongo Flava ni jumuiya kubwa, itumieni nguvu yenu kuendelea kuwapa nguvu vijana wengine wenye vipaji ili tuwe na wawakilishi wengi zaidi.

Kwakuwa bifu yenu inahusisha makundi makubwa yaliyo nyuma yenu ni ngumu kuimaliza kwa ushauri nasaha toka kwa mwandishi, mzazi, ndugu au mwingine, basi itumieni kushindana katika kazi, biashara na hadhi. Tunawapenda, hatupendi mchukiane kiasi cha kutisha hivi. Mungu awabariki. Amen .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad