Lowassa ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu.
"Kuna watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa" alisema Lowassa
Mbali na hilo Lowassa alisema kuwa licha ya mambo yote hayo lakini bado ukweli utabaki palepale kuwa Uhuru Kenyatta anapenda Demokrasia
"Tangu Demokrasia ya vyama vingi Uhuru Kenyatta hajaleta shida ya aina yoyote, siku moja nimeona kwenye TV yenu mama mmoja amemtukana mpaka matusi ya nguoni lakini asubuhi Rais anasema nimemsamehe bure, nawaambia huyu ndiye anawafaa, naondoka nikiwa na matumaini" alisema Lowassa
Siku ya Jumapili tarehe 8/8/2017 Wananchi wa Kenya watakuwa wakifanya uchaguzi kuchagua viongozi wao mbalimbali
Mwandishi naomba usahihishe kidogo tarehe 8/8/2017 ni jumanne pia siku hiyo kuna big match kati man u na real madrid samahani kwa usubufu
ReplyDeleteMauaji ya kutatanisha ya msimamizi mkuu wa IT wa Kenya bila shaka serikali ya kenyata imehusikka kwa njia moja au nyengine katika mauaji hayo sasa Lowasa anachokifuata huko kwa Uhuru kenyata kitu gani kama si kutojitambua? Utaona hapo ni jinsi gani Lowasa na chadema walivyo wanafiki kuhusiana na suala zima la demokrasia. Kule kenya hakuko vizuri katika huu uchaguzi na Mungu awajalie wamalize uchaguzi salama lakini lolote baya likiripuka kwenye huu uchaguzi basi Lowasa atahusika na umwagikaji wa damu za wakenya.

ReplyDelete