Godbless Lema Ashindwa Kunyamaza Kukamatwa Kwa Ester Bulaya, Adai ni Hatari Kwa Nchi

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Mh. God Bless Lema amelaani vikali kitendo cha Mbunge mwenzake Ester Bulaya wa Bunda kukamatwa na kuwekwa Rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya kwa madai kuwa hakuna sheria Tanzania inayokubali vitendo hivyo.

Akizungumza ofisini kwake mapema leo asubuhi, Lema amesisitiza kuwa vitendo hivyo ni muendelezo wa  uvunjifu wa amani huku akihofia kwamba nchi inapoelekea ni kubaya hasa mbegu za chuki ambazo zinapandikizwa zinaweza kuleta mpasuko mbaya katika taifa.

Mh. Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa mambo ya ndani amesema kuwa kosa lililomuweka ndani Mh. Bulaya la kushiriki mkutano wa hadhara uliofanyika Tarime halipo katika sheria ya Tanzania na hata ikifanyiwa marekebisho hakuna sheria inayomzuia mtu kuzungumza katika mipaka ya taifa lake.

"Kama mbunge niliyepitia madhila mengi yakiwepo ya kukamatwa na polisi mara kwa mara  hili jambo linasikitisha sana kwamba Mbunge amekamatwa kwa sababu ya kwenda kuhudhuria au kuhutubia jimbo lingine, Wakati Mbunge anaruhusiwa kuhutubia mahali popote ndani ya mipaka ya Tanzania ndiyo maana anaitwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata wewe Mwandishi au mtu wa kawaida. Hii ni hatari kwa nchi"
Tunapoelekea wasukuma watasema hawawataki wachaga usukumani yaani tutaanza kukataana. Hii mbegu siyo kwamba tu inauua demokrasia, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kutembea popote kama katiba inavyoainisha lakini kinatengeneza mpasuko mkubwa katika taifa. Mbegu hii ikiota italeta machafuko makubwa hapo mbeleni.

Lema ameongeza kuwa tabia zinazofanywa na viongozi wa serikali zinawapa nafasi wananchi kutenga watu kwa kabila zao, ukanda wao.

"Kitakuja kizazi ambacho hakitataka kuzungumza kupitia vipaza sauti au mitandao ya kijamii au kwenda kulilia kwenye mataifa mengine na badala yake vitafuata usemi wa jino kwa jino. Nazungumza hivi kwa sababu naipenda nchi yangu" Lema
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Amesungumusia Ofosini kwake au kure kwenye ire nyumba ya kubunge?? hii mapotesa ire mada kabiisa. nasungumusa ofyo ofyo kabisa . prereka kure rupango narisha bure narara bure. hapana achia mujini naenda na maji..magufuri oyee. napenda kabisaa magufuri yetu na tansania yetu. ya kasi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad