Grace Matata Awapa Somo Wasanii Kuhusu Mziki wa Live





Grace Matata Awapa Somo Wasanii  Kuhusu Mziki wa Live
Msanii wa Bongo Flava, Grace Matata ametoa somo kuhusu muziki wa live kwa kuwataka wasanii kujielekeza zaidi katika eneo hilo kama wanataka muziki wao kudumu muda mrefu na kuwa na heshima.



Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Dakika Moja’ aliyomshirikisha rapper Wakazi, ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa anapokuwa studio hujaribu kufanya muziki ambao akiwa katika jukwaa anaweza kuufanya live.

“Ukiangalia kwenye trend ya globally watu wanatengeneza pesa kwenye vitu tofauti kama downloads, endorsement lakini live performance bado ipo juu sana lakini kama umezoea kufanya kazi ya kawaida ukifika mahali umekuwa na jina kubwa unawekwa kwenye stage kubwa hapo ndipo utaelewa kwanini kuna umuhimu wa kuwa vizuri both one stage and off stage inakupa kind of respect,” amesema.

Amesema mwaka jana alipata bahati ya kuona performance ya Oliver Mtukudzi ambaye kwa sasa ana miaka 65 ila anavyofanya ni vigumu kuamini katika umri wake lakini siri kwamba amejijenga katika hilo miaka nendarudi.

“Mimi when I start hakuna kitu nilichokuwa naogopa kama kupanda on stage nikijua na event naumwa, nikafanya majaribio mpaka nikafanikiwa. For me I inspire kuwa very good performer na nina shauri kama wewe ni masanii na una mpango wa kwenda international kufanya big thing you have to do something about live performance vinginevyo itafika mahali unapewa platform unashindwa, ni muhimu sana,” amesisitiza.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad