Mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Grace Mugabe, ambaye anaomba kinga ya kidiplomasia kufuatia madai ya kumshambulia mwanamitindo, anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kikanda Afrika kusini baadaye leo.
Atashiriki mkutano huo wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), katika mradi wa wake wa marais, licha ya kukosa kujisalimisha kwa polisi baada ya kisa hicho kwenye hoteli moja Johannesburg mapema wiki hii.
Serikali ya Afrika kusini imekanusha madai kwamba ilipania kumkabidhi Bi. Grace Mugabe kinga ya kidplomasia baada ya kutuma ombi lake.
Polisi wameweka ulinzi mkali kwenye mipaka ya taifa hilo kuhakikisha kwamba Bi. mugabe hatotoroka.
Mwamitindo Gabriella Engels 20, alimshtumu Bi Mugabe 52, kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg
Bi Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.
''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo.
Grace Mugabe Kuhudhuria Mkutano wa SADC Licha ya Kwindwa na Polisi
0
August 19, 2017
Tags