HAKIKA Rais Magufuli si wa Kuchezea...Adai Mwizi ni Mwizi tu Hata Kama ni Mzungu......

RAIS John Magufuli amesema ifike wakati wizi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya viongozi wa serikali wakishirikiana na wawekezaji kutoka nje ukomeshwe ili kuleta maendeleo ya Tanzania kwa ajili ya wananchi wote na si watu wachache kujinufaisha.

Hayo ameyasema leo wakati akiwahutubia wanachi wa Hale wilayani Korogwe wakati akianza ziara yake ya siku tano mkoani Tanga ambapo atashirikiana na Rais Museveni wa Uganda kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani kwenye mwambao wa bahari ya Tanga, Agosti 5 mwaka huu.

“Mlinipa kura nyingi sana na ninawashukuru na ahadi yangu iko palepale kwamba sitawaangusha, unapokuwa na kiongozi anayewatumikia wananchi ni jambo nzuri.

“Hatukuumbwa kwa ajili ya kuwa wasindikizaji wa watu bali tumeumbwa ili kuwa Tanzania yenye neema ndiyo maana hata kwenye kutumbua majipu huwa sijali hata kama ni Mzungu. Wapo Wazungu waliokuwa wamezoea kutumbua dhahabu yetu, nimeamua kuwatumbua bila aibu ili kutengeneza rasilimali za Watanzania kwani mwizi ni mwizi tu, awe Mzungu, awe wa CCM, awe wa Chadema, awe wa CUF au hata kama hana chama.

“Nitasimama kwa ajili ya Watanzania wanyonge bila kujali itikadi zenu kwa sababu lengo langu mimi ni kuleta maendeleo,” alisema Rais Magufuli.

Aidha rais ameeleza kuwa kwa Afrika mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ni mradi mkubwa ambapo amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kupata maendeleo kwani watu zaidi ya 18,000 watapata ajira.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana Magu wetu. Tumekuchagua baada ya kukutathimini kwa kina. Ikiwemo utendaji wako na NIA NJEMA KWA NCHI YAKO. Baada ya kukuona ROha yayako ni ukarimu na Muadilifu hapo ndipo tulipo ridhika na kukupa kura zetu wote. TUNACHO KUOMBE NI MUNGU AKUBARIKI KATIKA KILA HATUA YA UJENZI WA MAENDELEO YA TAIFA LETU. NI KWELI TUNA WACHIMBAJI WENGI ASHANTI GGM NA AKASIA UKWELI WOTE NI LAZIMA TUWASHUGHULILIE KI LINA. SABABU WAO SIKU ZOTE WANAKUWA UNDER SHADOW NYUMA YA WATANzANIA WALAFI WENYE KAPENDA MASLAHI BINAFSI NA ULAFI AMBAO NI WABADHIRIFU. KWA HIYO WANATUMIA MADARAKA TULIO WAPA NA NAFASI ZA UONGOZI KUJINUFAISHA. HAO WOTE WALIKUWA WAPIGA DILI WAKA WA VIPINDI VILIVYO RUHUSU HALI YA HEWA KUCHAFUKA NA WATU KUTOELEWA AJILI YA HEWA . SASA MUNGU KATUBARIKIA KATULETEA MZIBA HEWA KILA TUNDU LINALOTOA HEWA. MWANA HALI YA HEWA KUIJUA KBLA YA DHORUBA KUFIKA MWAMBAO...BABA JPM.
    NI KWELI MZUNGU NI WEZI TENA WA HALI YA JUU ( DIGITALI NA SI ANALOGY) lakini bila ya kusaidiwa na Walafi na wabadhirifu(WATANZANIA WAPIGA DILI) hawawezi kwa hiyo WAO NO WIZI NA TUMEWASHTUKIA NA HAQA WAPIGA FIRIBI WA MAKINIKIA AMBAO WAMESHALISHWA PIA TUWAAHUGHULIKIE NA QENGI NI WANA SIASA UCHWARA TOKA CHAMA CHA UPANDE WA PILI AMBAO WAO NI WAPENDA UFISADI. MAGU MUNGU AKUWEKE NA UENDWLEE KUTUTUMIKIA. HONGERA SANA BABA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sawa kabisa mdau. MAGUFULI ni KIBOKO YAO. HANA UREMBAJI. ANAKUPA KESH CASH. NI MCHAPA KAZI NA MFATILIAJI VILIVYO.
      TUENDELEE KUMPA USHIRIKIANO KATIKA NYANJA ZOTE ZA UTENDAJI. MUNGU AMLINDE.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad