Maneno hayo ndiyo yamenifanya nikumbuke mpaka hadithi ya sungura baada ya kukosa ndizi kwa muda mrefu akajipa maneno ya kwamba "sizitaki mbichi hizi" nafikiri nitakuwa nimekukumbusha mbali kidogo juu ya hadithi hii.
Ndivyo hata sisi tumekuwa tukitumia maneno hayo, ndiyo ambayo yamekuwa yakijirudia kila siku katika maisha yetu, najua utakuwa unashangaa ila huo sio muda wa kushangaa bali ni muda wa kibatilisha maneno hayo, inawezekana nimekuacha kidogo ngoja nikukumbushe misemo hiyo au maneno hayo ambayo kimsingi yamekuwa yakikukwamisha kupata Mafanikio.
Ifuatayo ndiyo misemo ambayo inakukwamisha kupata Mafanikio.
1. Haraka haraka haina baraka.
Mara kadhaa umekuwa ukijaribu kufanya vitu vya msingi vyenye kukuletea manufaa ila kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanao kuzunguka wamekuwa wakiona kile ambacho unachokifanya mwisho wa siku kwa kuwa kina changamoto nyingi watakuambia maneno hayo kwamba haraka haraka haina baraka kwa kuwa wewe ndiyo mfanyaji wa jambo hilo unaamua kupunguza juhudi za kiutendaji wa jambo hilo.
Na ukichunguza kwa umakini wanaokwambia maneno hayo wao tayari wapo mahali fulani kimafanikio. Kumbuka kuwa kauli hiyo inazungumzia muda na muda haumsubiri mtu hata siku moja na moja ya uchunguzi ambao umewahi kufanywa juu ya muda waligundua ya kwamba kila mtu anayo saa lakini hana muda. Huo ndio ukweli watu kwenye simu zao wana saa lakini hawana muda wa kuleta mabadiliko binafsi na jamii kwa ujumla.
2. Pole pole ndio mwendo.
Hayo ni maneno ambayo umekuwa ukiishi nayo na kuamini kuwa kila kitu kitafanikiwa kwa hatua uliyo nayo. Ukweli ni kwamba kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha unafanya kwa uhakika na ufanisi wa kutosha ili kupata matokea.
Mara nyingi tumekuwa na maisha yaleyale kila siku kwa sababu unamini ya kwamba polepole ndio mwendo, huenda ikawa ni kweli. Ila tatizo linakuja kufanya vitu pole pole ambavyo havileti matokea chanya ya kimaisha, unajua kwa nini? kwa sababu unafanya mambo yako kwa staili ya aina moja.
Kwa mfano kama ni biashara umekuwa ukisubiria wateja tu na huna muda wa kuwafuata wateja harafu unasubiri hiyo pole pole iwe mwendo utasubiri sana.
Hata watu ambao wamefanikiwa na wao walikuwa wanaamini sana Kuwa pole pole ndio mwendo huku wakiongeza juhudi za kutaka kufanikiwa kwa kasi zaidi, na moja ya njia ambayo walizitumia ni kufanya kazi kama watumwa na leo hii wanaishi kama wafalme.
Hivyo ni muda wako muafaka na wewe kubadili njia za kutafuta mafanikio hayo tofauti na njia ulizozizoea.
Pia ni lazima ujue ya kwamba maneno yamekuwa yana nguvu sana. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kusema nipo nahangaika, ni kweli kama ni miongoni mwa watu ambao utahangaika sana. Badili tabia kauli zako kuanzia leo, utafanikiwa.
Nukuu ya Leo; chochote bila chochote huwezi kupata chochote.