Hili la Jackline Wolper Liwe Fundisho Kwetu Wanawake Wote Wanaopenda Serengeti Boys

Habarini za Weekend wanajamvi. Naomba niende moja kwa moja kwa Wanawake wenzangu wale Walioingia kwenye mtindo wa kuwataka au kuwakubalia Mahusiano ya Kimapenzi Wavulana wadogo alimaarufu Mario au Serengeti boys au Mwendo kasi kwa hapa kwetu Tz.

Jamani hawa vijana watawapeleka pabaya wanawake wengi mitaani nyumba zinaparaganika maelewano hakuna, mapenzi ya kawaida tu na Wanaume Watu Wazima nayo yanavunjika kitu mwendo kasi.

Naomba tuelewe ya kwamba hawa Wadogo zetu au Watoto wetu wavulana hivi Viserengeti viko kimasilahi zaidi wanataka kujikwamua kimaisha kutokana na hali ngumu mtaani wanatafuta kitonga eee upo hapo shoga. Wakisha timiza lengo lao au wakipata kitonga zaidi watakuacha kwenye mataa tena kwa aibu ujione kama Dunia nzima inakubana, atakutia stress na kukuhujumu kama siyo kukufilisi. Kikubwa hata shukrani hawana. Tofauti na mwanaume mtu mzima Mara mia atakuonea huruma kwanza yeye mwenyewe anajiona fahari kuwa nawe.

Mwanamke unaweza kosana na Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya havi vitoto jamani. Tafadhali tujitathimini kwa kina kabla ya kujitumbukiza kwenye Mahusiano na Wavulana Wadogo WA Shule, Bodaboda, Madereva Bajaji, Wasafisha kucha, Wauza urembo n.k tutakuja kujutia maishani na kuona kama tumedhalilika.

Nimpe pole tu mdogo wangu kiumri Jackline Wolper  Yaliyopita si ndwele agange ya jayo kwa kuwa ameamua kuongea basi ameshapona maana katua zigo kifuani na moyoni, ni wakati wake sasa kuwa na mtu WA heshima kama yeye atulie nae ana kila kitu cha kuitwa "Wife Material" hana haja ya kuhangaika na hivyo vitoto vya Jana havijui hata maana ya namna ya kutumia K na Wapenda miserereko. Maisha bado yanaendelea na Watu wengi bado tunampenda kwa jinsi anavyojituma kutafuta maisha atumie njia halali inayompendeza Mungu atapata faraja ya milele , Amina.

Basi ni hayo tu nimeona ni-share nanyie wapendwa. Samahani kama kuna mtu itakuwa nimemkwaza kwa namna yoyote ile siyo kwa makusudi Bali ni kuelimishana tu " Wanawake majanga yetu yanakaribiana, Kitabu chetu ni Kimoja na Mungu wetu ni mmoja yule wa Huruma na Upendo".
Karibuni.

TAZAMA YALIYOMPATA JACK WOLPER HAPA CHINI:

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mie naona kama anazungumza kwa msukumo wa Ulevi flani. Millard hembu sema kweli. Sisi mashabiki zake tunataka kujua.Queeni wetu alikuwa na haligani ulipokutana nae?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad