Huto Amini Hii Ndio Idadi Kamili ya Watu Waliouawa Kutokana na Vurugu za Uchaguzi Kenya....


Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya (KNCHR) imesema kuwa watu 24 wameuawa tangu kuanza kwa kipindi cha uchaguzi tangu Agosti 8.

Katika taarifa iliyotolewa na tume hiyo imeeleza kuwa watu 17 wameuawa katika mji wa Nairobi City, Homabay wameuawa 2, Kisumu ameuawa 1, Migori 2 na Siaya wameuawa watu 2.

Wakielezea chanzo cha mauaji hayo, tume hiyo ilisema wengi wameuawa kwa kufyatuliwa risasi wakati wakiandamana katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Taarifa hiyo imekuja wakati chama cha upinzani kimesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa lakini hawakutoa uthibitisho wowote wa madai hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad