Huu ni Uamuzi wa Mahakama kwa Chidy Benzi Baada ya Kukamatwa na Madawa ya Kulevya
0
August 17, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewaweka chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka miwili Msanii wa Bongofleva Rashid Abdalah maarufu Chidbenzi na wenzake watano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo dhidi ya maombi hayo.
Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo hicho kwamba mahakama iwaweke chini ya uangalizi baada ya kubainikia kujihusha na matumizi ya dawa za kulevya.
Maombi hayo yalisikilizwa na kutolewa uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mfawidhi Ritha Tarimo. Mbali na Chidi Benz, wengine watakaokuwa chini ya ungalizi ni, Hadia Abeid, Said Ally, Athuman Elias na Hassan Mohamed.
Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa upande wa Jamhuri unawasilisha hati ya kiapo kutoka kituo cha polisi Msimbazi kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya hivyo mahakama itoe dhamana kwani wamekuwa na tabia mbaya katika jamii.
Glory alidai kuwa wanaiomba mahakama itoe amri ya kuwaweka wajibu maombi chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu na kusaidi dhamana ambayo itahakikisha wanakuwa na tabia njema na kutojihusisha vitendo vya dawa za kulevya.
Akitoa uamuzi hakimu alisema wajibu maombi watakuwa chini ya uangalizi wa polisi miaka miwili na kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaotia saini ya dhamana ya Sh.milioni mbili kila mmoja na kuripoti kituo cha polisi Msimbazi kwa mwezi mara moja.
Tags