Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba tayari miili ipo wenye utambuzi kwa kuchukua vinasaba ili kujua ni raia wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao kwenda kuangalia kama ni wao.
Kamanda Siro aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kwamba watu wanafikiria mauaji hayo yamefanywa na Jeshi la Polisi, wafahamu kwamba wao kama Jeshi la Polisi huwa hawana kificho, kama wamekutana kwenye mapambano wamewaua watu wataweka wazi kuwa wameua, na siyo kwenda kuwatumbukiza baharini.