IGP Sirro Atoa Onyo kwa Polisi na Kuwataka Kufanya Kazi kwa Kutenda Haki

IGP Sirro Atoa Onyo kwa Polisina Kuwataka Kufanya Kazi kwa Kutenda Haki
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili Arusha na kuwabadilikia baadhi ya polisi na kuwataka kufanya kazi kwa kutenda haki pasipo kujali rangi ya mtu pia amewaonya polisi waonaokwenda kinyume na utaratibu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Sirro amewataka polisi wanaokwenda kinyume na utaratibu wa jeshi hilo kuacha mara moja na kuwakumbusha kutenda kazi pasipokumuonea mtu ili kutenda haki kwa wananchi wote na kuleta usawa na kudai yoyote atakayebainika kwenda kinyume na utaratibu hatua zitachukuliwa ikiwemo kushtakiwa kijeshi.

Mbali na hilo IGP Sirro amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kupata taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu kwa wepesi zaidi.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad