Kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na kama ni kweli kwamba watu ambao ni wembamba ni bora zaidi ya watu wanene. Nimelazimika kufanya utafiti kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania ili kujua ukweli kwenye hilo.
Jibu nililopata ni kwamba kwa asilimia kubwa kuna ukweli; kwamba walio na wembamba wana uwezo wa kukimbia masafa marefu zaidi ya wale ambao ni wanene. Japo wanaweza kujitetea, siyo wanene wengi wenye uwezo wa kukimbia masafa marefu.
Suala la mahaba linahitaji kutumia akili zaidi ya kufikiri kwamba utamridhisha mwenzi wako kwa sababu wewe ni mwembamba au mnene.
Ni wanawake wa aina gani wanavutia zaidi katika suala la mahaba? Utafiti unaonyesha kuwa walio wembamba wana raha yake kwa sababu furaha ya wanaume wengi ni kudumu katika mahaba kwa muda mrefu, kwa hiyo walio wembamba wengi huwa hawachoki kwa haraka; miili yao haina mafuta mengi ya kuwachosha.
Walio wembamba wanaweza kukuruka huku na kule, wakati kwa wanene, kuna baadhi ya mambo hawawezi kwa sababu ya namna walivyo. Japo wapo wanene, na wana uwezo wa kwenda huku na kule, siyo wengi, kama walivyo watu wembamba.
Ni vigumu kuandika kwa kina, lakini kuna baadhi ya miondoko, watu wanene hawawezi. Kauli kama nimechoka huwa ni nyingi ukilinganisha na walivyo watu wembamba.
Hata hivyo ninapozungumzia watu wanene nazungumzia wale ambao hata kutembea kwao ni shida, kwamba wana unene wa kupitiliza. Kitaalamu huwa inashauriwa kuwa na ‘nyama’….godoro linalobonyaa-bonyaa huwa ni zuri kuliko lile ambalo gumu sana…si ndiyo jamani?
Mwanamke kwa mwanaume, unapaswa usiwe mkavu sana, maana kama ukiwa mkavu sana inasababisha maumivu, maana unaguswa na mifupa hadi inatia maumivu badala ya raha. Ninachotaka kusema ni kwamba wanandoa wanapaswa kuhakikisha wanakula, wanaondoa msongo wa mawazo nk ili wawe na miili inayonawiri….kuwa na mwenzi ambaye mwili umebaki mifupa…Mhh mnakuwa mnasababishia maumivu jamani…!
Ndiyo ukweli wenyewe
Wanawake wengi wembamba ni watalamu wa mapenzi kuzidi wanawake wanene, hii inatokana na tafiti mbalimbali zilizofanya na watalamu wa masuala ya mapenzi kama wakina Leticia Jackson wa Marekani, Prof. Benjamin James wa Ufaransa, Dk. Edward Hulow wa Uingereza.
Wataalamu hawa katika tafiti zao walizofanya katika nchi mbalimbali zinaonyesha kuwa asilimia 85 ya wanawake wembamba wanajua miundo mingi wakati wa chakula cha usiku. Hawa walio wengi, kabla ya kukutana nao inabidi ule ugali na nyama kavu…ukila chips kavu unaweza kujikuta unaanza kudanganya aaah unajua kazini kuna kitu nimesahau….aaah nahisi kiuno kinauma nk.
Utafiti unaonyesha asilimia 15 ya wanawake wanene ndio wanaojua kushiriki vizuri katika mahaba. Sababu inayofanya wanawake wembamba kuwa wataalamu sana ni kutoka na wepesi walionao.
Ni kutokana na wepesi wao, wanaweza kujikunja na kukaa namna yoyote.Japo siyo kila mwanamke anaweza kufanya hivyo katika mapenzi wengine hawataki hata kutoa ushikiano katika mapenzi. Kuna wengine ni wembamba lakini mizigo, kila unachomwambia anakwambia siwezi.
Kama mpenzi wako anafanya hivyo na huipendi hiyo tabia ni bora umwambie au umfundishe, kwa sababu siyo kila mtu anajua kila kitu japo kuwa kila mwanaume ana uchaguzi wake ila uchaguzi wako isiwe sababu ya kuwanyanyapaa wanawake ambao siyo chaguo lako.