Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limetoa onyo kwa watu wanaopiga picha za utupu na kuzirusha mitandaoni, huku likisema kuwa litawachukulia hatua watu hao kwani wanavunja sheria.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa, amesema vitendo hivyo ni uvunjaji wa sheria za makosa ya kimtandao na haviwezi kuvumilika.
“Hilo ni kosa kama kosa lingine, ni uvunjaji wa sheria za makosa ya kimtandao, mtu yeyeote akija kulalamika Jeshi Polisi halitalifumbia macho, kwa sababu vitendo hivyo ni udhalilishaji wa utu wa mtu wa hali ya juu na haviwezi kuvumilika, ukithibitika unafanya kitendo hicho Jeshi la Polisi halitakuacha salama, litakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”, alisema Kamanda Mambosasa.
Vitendo vya upigwaji wa picha za utupu na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii vimekuwa vikishamiri nchini Tanzania, ambapo hivi karibuni msanii Amber Lulu alifikishwa katika kituo cha polisi cha Ubungo kwa kosa hilo