Kagame Awaponda Wazungu Katika Sherehe za Kuapishwa




Kagame Awaponda Wazungu Katika Sherehe za Kuapishwa
Rais Paul Kagame wa Rwanda jana amliapishwa kuongoza taifa hilo kwa miaka mingine saba baada ya kushinda kiti hicho kwa asilimia 98 katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni.
Akihutubia baada ya kuapishwa, Kagame alikemea Mataifa ya Magharibi yanayokosoa Afrika na kuilazimisha kufuata mitindo na mifumo ya utawala wa Kimagharibi huku akiwaasa viongozi wa Afrika kupigania kujiwezesha kwa mataifa yao kama linavyofanya taifa lake.

 Marais kutoka nchi 19 za Afrika walishiriki akiwemo, Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye alichaguliwa tena Agosti 8 kuendelea kuiongoza nchi hiyo baada ya kumshinda Raila Odinga.
Wengine ni marais na Wakuu wa Serikali za Mataifa ya Afrika waliohudhuria sherehe hiyo, alikuwepo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilimtuma Spika wa Bunge Obe Minaku nayo Tanzania ikawakilishwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa. Burundi haikuwakilishwa lakini alikuwepo Rais wa zamani Pierre Buyoya aliyealikwa miongoni mwa marais wastaafu.
Rais Kagame alieleza kuwa miaka 23 baada ya Rwanda kukumbwa na mauaji ya kimbari wananchi wake sasa waliamua kujenga taifa linalojiwezesha.

“Tulilazimika kupambana ili kulinda haki zetu na kufanya kile ambacho ni kizuri kwetu na tutaendelea kufanya hivyo. Lakini Rwanda haiwezi kuwa mfano pekee lazima kila mwananchi wa Afrika, kila taifa lipiganie kuishi bila kuetegemea wengine au bila kujali wengine wanavyotaka. Wanataka mifumo inayofanya kazi vizuri kwetu tuibadilishe na mifumo yao ambayo wananchi wao wameanza kupoteza imani nayo,” alisema Kasgame.

Mara tu baada ya uchaguzi kufanyika Marekani ambaye ni mshirika wa karibu wa Rwanda licha ya kupongeza wananchi wa Rwanda kwa uchaguzi nchi hiyo ilisema kulikuwa na dosari zilizojitokeza kabla na wakati wa uchaguzi.
Isitoshe nchi hiyo ilipokea shingo upande mabadiliko ya katiba yaliyompa fursa rais Kagame kugombea muhula wa tatu madarakani.
Rais Kagame hakutaja ajenda yake ya miaka 7 ijayo, lakini baadhi ya wananchi wameeleza kufurahishwa na mafanikio ya utawala wake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad