Kauli ya Ayoub Mohamedi kwa Watumishi wa Serikali Wasioendana na Kasi ya Rais Shein Watakiwa Kuacha Kazi

Kauli ya Ayoub Mohamedi kwa Watumishi wa Serikali Wasioendana na Kasi ya Rais Shein Watakiwa Kuacha Kazi
Kauli hiyo ameitoa mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Zanzibar Ayoub Mohamed Mahamoud mbele ya Waandishi wa habari kuwa kwasasa Serikali yake ya mkoa haitaweza kumvumilia mtumishi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa wakati na hivyo kuwataka wajitathmini wenyewe.

"Nataka nieleze, kwa watendaji ambao wanaona hawaendani na kasi yangu na ya Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein waanze kuachia ngazi wenyewe... Hatutaweza kumvumilia mtu yoyote anayekwamisha" Alisema RC Ayoub

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rais Shein kutoa maagizo 13 kwa mkuu huyo wa mkoa na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati.

RC Ayoub amesisitiza kuwa kila kinachofanyika kwasasa ni lazima kiende kwa kasi na kwa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa ofisi yake sasa inaanza mchakato kutathmini ili kubaini watendaji hao mara moja.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msijigambe hamna kasi hata moja, kwani kasi nongo kila mtu anazo?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad