KAULI ya Serikali Kuhusu Wanafunzi Kwenda Vyuo Vikuu Bila Kuhitimu Kidato cha Sita....
0
August 20, 2017
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuutarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari
“Serikali yapiga Marufuku Kusoma Shahada bila kupita Kidato cha Sita,” tarifa hiyo siyo ya kweli na haijatolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako.Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako hajatangaza popote na kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.
Profesa Ndalichako yuko Mkoani Kigoma kwenye ziara ya ufuatiliaji wa Miradi ya Elimu, inayotekelezwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara yake.
Vile vile Wizara inapenda kutoa wito kwa watanzania kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuupotosha umma kwa taarifa ambazo siyo sahihi na hazina ukweli wowote.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina utaratibu wake wa kutoa taarifa hivyo inawaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kutokana na kusambaa kwa taarifa hiyo.
Imetolewa na:
Mwasu Sware
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
19 Agosti, 2017
Tags