KIBAHA: Wachina Wadaiwa Kupiga 'Dili zito' Ujenzi wa Stendi Mpya ya Mabasi

Wananchi wa Mji wa Kibaha Mkoani pwani wameilalamikia kampuni ya M/S Group Six LTD inayojenga Stendi mpya ya mabasi kuwauzia kifusi cha mchanga ambacho halmashauri ya mji huo ilitoa bure kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa kituo hicho.

Kwamujibu wa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Kajumbo kutoka kampuni mzawa wa MEG Business Solution ameeleza kuwa Wachina hao wamekuwa wakiwatoza kiasi cha shilingi Elfu 5,000 hadi elfu 20,000 ili kupata kifusi hicho jambo ambalo ni kinyume cha Agizo la mkurugenzi wa  Halmashauri ya Mji wa Kibaha

Hata hivyo Rashid ambaye tayari alikuwa na kibali cha mkurugenzi mkononi cha kupewa kifusi hicho bure amesema magari yake manne yaliyo katika eneo la mradi wa Stendi hiyo inayojengwa karibu na Karakana ya Serikali hato yaondoa mpaka Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa atakapofika katika eneo hilo na kuelezwa jambo hilo.

Baada ya madai hayo Mtandao huu umemtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo kwa njia ya simu ambaye amesisitiza hafahamu chochote kuhusu hilo ingawa anatambua kifusi hicho kinatakiwa kutolewa bure na hivyo amefahamisha kuwa anafuatilia kama Kampuni hiyo inawauzia wananchi kifusi hicho.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nchi hii majungu yametamalaki.kwani umelazimishwa kununua kifusi cha wachina. Katafute cha bure sehemu nyingine brrrr

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe sio yametamalaki. Hao wachina wamepewa tenda tu Yaani kazi wafanye na mwisho wa siku wanalipwa chao, ni kheri wangekuwa wazawa wa nchi hii, Lakini ni wageni. Raslimali ni Mali za wenyeji wa hapo Sio wachina, wachina raslimali zao ziko kwao. Kama hakuna kwa kupeleka huo mchanga si hela zinaenda kwenye almashauli, Sio mikononi kwa wachina. Au wapewe bure tu, na hela zao wenyeji wakawanunulie chakula watoto wale washibe waepukane na kwashakoo au utapia mlo, Jaamani Mtoto wa Africa nae lini atajisikia naye ni mkazi wa ulimwengu huuu!! Wachina watoto wao wanakula vizuri huko, mtoto wa Africa utapia mlo mmmmmh.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad