Kibano Kingine...Manispaa ya Ilala yapiga Marufuku Kuosha Magari Pembeni ya Barabara

Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam imesema kila kijana atakayekutwa anaosha magari pembezoni mwa barabara za manispaa hiyo atapigwa faini ya shilingi laki mbili papo hapo huku mmiliki wa gari husika nae akitozwa faini kama hiyo.

Aidha Mkurugenzi wa mazingira amesema licha ya kupigwa faini kwa watu hao lakini bado watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Mkuruegenzi wa mazingira na udhibiti wa taka katika manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda amesema kumezuka tabia kwa baadhi ya vijana kugeuza maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo kuwa maeneo ya kuosha magari huku maji wanayotumia yakitiririka barabarani na kusababisha kutuama jambo ambalo ni uchafuzi wa mazingira.

Amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo mwezi Juni mwaka huu wameshafanikiwa kukamata vijana hao pamoja na wamiliki wa magari wasiopungua 50 na kuwapiga faini pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad