Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Halima Mdee ameijia juu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) na kusema bodi hiyo inataka kukandamiza elimu sekta ya elimu kwa kufanya ubaguzi.
Halima Mdee amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandish wa habari katika Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam
"Kifungu cha tisa kinasema kuwa waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi katika makampuni binafsi yanatotambulika na mamlaka za mapato na usajili hatarajiwi kuomba, lakini kifungu cha pili cha kumi kinasema waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa Umma, au kisiasa ambao wanatajwa na sheria ya maadili na viongozi wa umma na wenyewe hawatarajiwi kuomba mikopo, sasa watu wa kawaida wakisikia viongozi ambao wanajaza fomu za maadili wanajua labda kwenye ubunge au mawaziri lakini hata katika hizo gazi za ubunge, uwaziri au mameneja unamnyimaje mtu haki yake ya Kikatiba ya mtoto wake kupewa fursa ya elimu sambamba na mikopo kwa kudhania kwa kuwa mtu huyo ana nafasi hiyo anaweza kulipa utajuaje pengine mtu huyo analipia watoto kumi au ishirini kwa mwaka" alihoji Halima Mdee
Halima Mdee amedai kuwa wanatumia hoja nyepesi na hovyo zisizo na mantiki kuwabagua watu kielimu
"Wakati UKAWA tunaeneza Ilani yetu tulisema kuwa tutatoa elimu bure mpaka Chuo Kikuu pasipokubagua kwa sababu ni jukumu la serikali kutoa elimu kwa watoto wake, sasa wenzetu wao wanaotuambia kila mwezi mapato TRA yanakuwa wanaanza kutapatapa yaani wali copy na kupaste sera ambayo hawawezi kutekeleza sasa hivi wanaanza kutumia visingizio kuanza kubagua Watanzania, sasa hili suala tutalikemea na kuendelea kukemea" alisema Halima Mdee
Siku ya Jumamosi ya tarehe 5 Agosti mwaka huu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) imetoa mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ambapo bodi hiyo imeanza kupokea kupokea maombi ya mikopo kuanzia tarehe 6 Agosti 2017 hadi tarehe 4 Septemba, 2017.