Kisa Kutoa Siri ya Ndege "Tundu Lissu Atishiwa Kifo"

Baraza la Vijana Chadema limedai Serikali inahatarisha maisha ya Mwanasheria wa Chadema, Mh. Tundu Lissu  kwa kudai kuwa kiongozi huyo ni adui wa nchi na Mhujumu wa nchi imesababisha kupata tishio la uhai wa maisha yake.

Akiwawakilisha vijana wa Chama chake Mwenyekiti Patrobas Katambi amesema kuwa kutokana na kauli iliyotolewa baada ya Lissu kutoa siri za kukwama kwa ndege aina Bombadier Q400 nchini Canada watu walioelewa kauli za serikali tofauti wameahidi kumtoa uhai Kiongozi huyo kwa kuomba ruhusa ya kukamilisha kukatisha uhai wa Tundu Lissu.

"Zipo akili za watu wachache ambao kauli ya serikali iliyotolewa wameielewa jinsi ambavyo wao wameelewa. Kupitia mitandao ya kijamii tumekutana na Watanzania walioonyesha hisia zao kuhusu kauli ya Lissu kufuatia kauli ya Serikali kusema kiongozi anahujumu nchi na makosa yake yametajwa zaidi ya uhaini. Sasa sijui kama watampatia ulinzi maana uhai wake upo hatarini. Sasa huyu kijana hatuwezi kumtaja jina ameomba ruhusa kutoka mamlaka ya juu kupitia mitandao ya kijamii aweze kumuua Lissu je ni wangapi wenye akili kama hizi ambao hawajaomba ruhusa?
Akizungumzia kuhusu kamata kamata zinazofanywa na polisi kupitia wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, Katambia amesema viongozi wa juu wapo tuu wanaangalia uvunjifu wa sheria kwa jinsi unavyofanywa pasipo kufanya jambo lolote kwa kisingizio cha agizo kutoka juu.

"Unaweza kuona wabunge wa upinzani jinsi ambayo wanapelekwa, Lissu hii ni mara ya 11 anafikishwa polisi, Bulaya mpaka ameugua akiwa rumande lakini pia CHADEMA tuna kesi zaidi ya 301 za viongozi wanachama na wafuasi wengine lakini zote ukifuatilia hakuna kesi za msingi. Sisi Vijana tumechoka na tunaomba kufahamu huko juu ni wapi au ni nani?

Akimzungumzia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti Katambi amesema anashangaa kumuona kiongozi huyo akiwa amenyamaza kimya wakati mambo hayo yakifanyika badala ya kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya kumsaidia Mhe. Rais kama askari wanafanya makosa lakini yeye kakaa kimya kama wizara yake haina mtu.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. eti jamani si raisi pia huwan ana sema msema kweli ni mpenzi wa mungu kwa hio kwa nini wamshike wachen uonevu bwana

    ReplyDelete
  2. sasa huyu si binadamu na raia. mwisho wake binadamu ni nini? sasa cha ajabu au kushtushwa ni kipi. KIFO NI WAJIBU NA SISI WOTE TUO KATIKA NJIA HIYO.
    BAVICHA WACHENI VIOJA. WEWE TAKUFA NA LISU NA MIMI QOTE TIKO NJIANI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad